Thursday, November 2, 2017

Ujumbe wa Muhammad haukutoka kwa Mungu wa kweli


 

Muhammad si tu kwamba ni mtume ambaye hashuhudiwi na binadamu mwingine yeyote bali pia namna alivyokuwa akipata ufunuo (wahyi) wake ni jambo linalotia mashaka makubwa sana.

Hashuhudiwi na binadamu mwingine yeyote kwa sababu mambo yote aliyosema yanatoka kinywani mwake peke yake na hakuna mtu wa pili wa kusimama kama shahidi ili kuonyesha kuwa alichosema ni kweli kinatoka kwa Mungu wa mbinguni.

Yaani shahidi wa mambo yake ni yeye peke yake.
Na hakimu wa mambo yake ni yeye peke yake.


Kuhusu namna alivyokuwa akipata hayo mafunuo yake, hebu tuangalie suala la yeye na wanawake.

Muhammad alisema kapokea ufunuo kwamba mwislamu anaruhusiwa kuoa wake hadi wanne.

Lakini kuhusu yeye, ufunuo ulisema hakuna mipaka juu ya idadi ya wanawake anaowataka.

Mmojawapo wa wake wa Muhammad aliitwa Hafsa.
Hafsa alikuwa na mtumwa au mjakazi wa kike aitwaye Mariyah.

Siku moja Muhammad alikwenda kwa Hafsa.
Alimwona Mariyah.
Akamtamani.

Ikabidi amwambie Hafsa kuwa baba yake anamuita (lakini haikuwa kweli).
Hafsa alipoondoka, Muhammad alifanya juu chini akalala na Mariyah.
Hafsa alipokuja, akajua na akachukia sana.

Muhammad akambembeleza kwamba hatarudia tena kufanya jambo hilo.

Lakini baadaye, ikaja aya inayosema:

Ewe Nabii! Kwa nini unaharimisha alicho kuhalilishia Mwenyezi Mungu? Unatafuta kuwaridhi wake zako. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. (Quran 66:1).

Hapa ndipo mtu unajiuliza:
1.     Kama mungu huyu anajua kuwa alichofanya Muhammad ni dhambi – ndio maana anasema “Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu”, kwa nini alete aya kama hii?
2.     Kwa kuwa hakuna ushahidi (kama kawaida) kutoka kwa mtu mwingine yeyote juu ya hili zaidi ya maneno ya Muhammad peke yake, je, haiwezekani kwamba Muhammad alikuwa akitengeneza aya hizi mwenyewe ili kuhalalisha mambo yake?
3.     Na kama alikuwapo aliyekuwa akizileta, je, hii si ishara kwamba allah sio Mungu wa kweli bali ni kitu kingine tu tofauti?

Si mimi peke yangu mwenye mawazo kama haya. Hata wake zake Muhammad nao walikuwa wakiingiwa na mashaka kutokana na staili hii ya Muhammad ya kuleta aya ili kujiokoa na kujihalalishia mambo aliyokuwa akiyafanya. Hata mke wake kipenzi sana, Aisha aliwahi kusema:

I said (to the Prophet), "I feel that your Lord hastens in fulfilling your wishes and desires." (Sahih Bukhari 60:6:311)

Yaani:
Nilimwambia Mtume, “Nahisi kama Bwana wako anaharakisha kutekeleza matakwa na matamanio yako.

Yaani aliona kwamba, mbona huyu bwana kila akifanya jambo, tukihoji tu, hachelewi kuja na aya? Kuna nini hapa?

Lakini sasa Aisha angeenda kumwuliza nani?
Maana shahidi ni yeye (Muhammad)
Na hakimu ni yeye.

Kibiblia, inajulikana kuwa Mungu anasema katika Kumb 19:15
jambo na lithibitishwe kwa vinywa vya mashahidi wawili, au watatu.

Ndio maana Mungu wa Biblia alituma manabii walioishi
-       nyakati tofauti
-       nchi tofauti
-       wenye elimu tofauti
-       wenye lugha tofauti
Lakini unaposoma vitabu vyao unagundua kuwa ujumbe wao unaoana kabisa.
Na ndio maana siku za leo baada ya vitabu vile kukamilika, tunambaini mara moja nabii wa uongo pale tunapogundua anachokisema kinapingana na Biblia.

Muhammad kwa mujibu wa Biblia si nabii wa kweli hata kidogo.
Na kwa msingi huo, hajatumwa na Mungu bali asili ya ujumbe wake umetoka kwingineko tu.
Tafakati.
Chukua hatua.
Yesu peke yake ndio njia, kweli na uzima.

No comments:

Post a Comment