Friday, November 10, 2017

Wanadai "Eloi" ndio Allah


Ndugu zetu Waislamu wanadai kuwa Mungu wa Yesu ni Allah wao wanayemwabudu.

Mojawapo ya utetezi wao ni kuwa jina “Allah” ndio lilelile aliloita Yesu pale aliposema “Eloi, Eloi, lama sabakthani”.

Yaani kwa vile “Eloi” inakaribiana kimatamshi na “Allah” basi ndio kwao ni sababu kuwa Allah ndio Eloi.

Lakini hebu tujiulize swali hili la mfano:
Kama mimi nikikuambia kuna maduka mazuri sana kwenye sayari ya jupita hii suruali nimeinunua kule; nipe fedha nikienda nitakununulia. Je, utanipa?
Naamini hutafanya hivyo kamwe.
Kwa nini?
Kwa sababu moyoni MWAKO unaamini kabisa kuwa mimi nakudanganya.
Je, waweza kumshauri mtu mwingine anipe fedha huku ukimwonyesha suruali yangu kama ushahidi wa kwamba mimi nilienda kwenye sayari ya jupita kununua nguo?

Naamini hutafanya hivyo kamwe.
Kwa nini?
Kwa sababu moyoni MWAKO unaamini kabisa kuwa mimi sijaenda huko.

Sasa cha ajabu ni kuwa, Waislamu WOTE pamoja na Mungu wao wanaamini kuwa Yesu hakuwambwa msalabani na wala hakufa.

Kwa kuwa wanaamini hivyo, maana yake ni kuwa, kwa kuwa Biblia inasema katika Mathayo 27:44-46

Pia wale wanyang'anyi waliosulibiwa pamoja naye walimshutumu vile vile. Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa. Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani?

Sijui kama umeona kitu hapo? Yaani Yesu alitamka maneno hayo (Eloi, Eloi, lama sabakthani) akiwa MSALABANI ameshasulubiwa.

Sasa kama nyie Waislamu HAMUAMINI kwamba Yesu aliwahi kusulubiwa, mnawezaje kuamini kwamba aliwahi kutamka maneno hayo akiwa msalabani; na ajabu zaidi mkayatumia kama ushahidi wa kumthibitisha Mungu wenu?

Kwa hiyo, hoja yenu kwamba Allah ndio Mungu wa Yesu haina maana, mantiki wala uzito kwa sababu imejengwa juu ya kile mnachoamini kuwa ni uongo.

Na hata hoja ya kudai eti, “Sisi tunatumia kile mnachoamini nyie ili kuwathibitishia mambo” ndio kabisaa haina mantiki hata kidogo hapa.

…………

Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo SIO allah wa waislamu.

No comments:

Post a Comment