Friday, November 10, 2017

Yesu sio Mtume tu. Usijidanganye?




Ndugu zetu Waislamu wamefundishwa kwa Yesu ni Mtume tu na ni mwanadamu tu kama binadamu wengine. Wamekataa Uungu wa Yesu na ukuu wake, huku wakidai kuwa Yeye ni sawa tu na Adamu. Je, ni mwanadamu gani aliwahi kuwa na sifa hizi?



Yesu akasema katika Yohana 14.13
Nanyi mkiomba LO LOTE kwa jina langu, hilo NITALIFANYA.
-       Hapa Yesu hamaanishi wakati ule, bali SASA.
-       mwanadamu gani anaweza kuombwa LOLOTE?
-       Mwanadamu gani anaweza kufanya kila anachoombwa?
-       Hata kama ungesema anafanya kwa uwezo wa Mungu, je, Muhammad, Musa, Daudi au yeyote anaweza kuombwa LEO hata jambo dogo akalifanya?

…………

Yesu akasema katika Mathayo 18.20
Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.
-       ni mwanadamu gani anaweza kuwa KILA MAHALI duniani kwa wakati mmoja.
-       Je,ni Muhammad, ni Musa, ni Daudi?

…………..

Yesu akasema katika Marko 28.20
na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
- Je, ni mwanadamu gani anaweza kuwapo WAKATI WOTE hadi mwisho wa ulimwengu?

…………..
Ni Yesu TU aliye na uwezo wa kuwaandali wanadamu wote MAHALI PA MILELE.
Yesu akasema katika Yohana 14:2 – 3
maana naenda kuwaandalia mahali. …. nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
-       ni mwanadamu gani mwenye uwezo wa KUWAANDALIA wanadamu wanaokufa mahali pa kukaa?
-       Ni Muhammad au Musa?

…………………
Ni heri ungeamka leo.
Hakuna uzima KAMWE nje ya Yesu Kristo.
Asante Yesu, Mungu wa mbingu na nchi.

1 comment:

  1. Golden Nugget Resort Casino - Mapyro
    Golden Nugget Resort Casino. 과천 출장샵 Las Vegas, NV 89135. Directions · 경주 출장샵 (702) 849-1000. Golden Nugget. Hours. 공주 출장안마 Accepts 구미 출장안마 Credit Cards, Cards, 하남 출장샵 Pays/

    ReplyDelete