Mhalifu wa kidini akihukumiwa kwa mujibu wa sharia [Kama unachofanya ni kizuri; ni cha Mungu, kwa nini ufiche uso?] |
Waislamu Wanazidi kukutana na Yesu
na Grantley Morris
‘. . . shuhuda zaidi na zaidi zinakuja kutoka kwenye nchi
zilizofungwa juu ya Mungu anavyowapa Injili Waislamu kwa namna isiyo ya kawaida
kupitia ndoto na maono. Miongoni mwa maelfu ya waamini katika Irani katika
miaka michache iliyoisha, zaidi ya nusu yao wamekuwa waamini baada ya Yesu
mwenyewe kuwatokea katika ndoto au maono.’ Wendell Evans wa the Billy Graham
Center’s Institute for Muslim Studies anazungumzia juu ya wingi wa ndoto na
maono yanayoripotiwa kuhusu Kristo miongoni mwa Waislamu . . .’
Kuzimu
Abdullah alikuwa Mwislamu mwaminifu. Aliishi umbali wa
kama saa moja hivi kwa mwendo wa gari kutoka Makka. Alikuwa akiswali mara tano
kwa siku, na mara kwa mara alitembelea Makka.
Kama ilivyo kwa Waislamu wengi, Abdullah alifundishwa kuwa
Wakristo wana pepo wachafu na kwamba anatakiwa kujiepusha nao.
Usiku mmoja Abdullah aliota ndoto kwamba yuko kuzimu,
anaungua moto. Asubuhi iliyofuata, akiwa ana wasiwasi mkubwa, aliomba kwa Allah,
‘Nimefanya kila kitu vizuri; kwa nini niende motoni?’ katika ziku zilizofuata,
aliendelea kupata wasiwasi zaidi.
Siku moja alishindwa kulala kabisa kwa sababu ya hofu. Usiku
ule kulitokea mwanga mkali ulioangaza chumba chake na akasikia sauti inasema, ‘Mimi
ni Yesu. Njoo kwangu. Mimi ni njia ya kwenda mbinguni. Nifuate mimi nawe
utaokolewa na ule moto.’ Abdullah alianguka chini huku akilia na akasema, ‘Tafadhali,
nisaidie namna ya kukupata.’
Baada ya siku chache Abdullah alipata Biblia na akaanza
kuisoma. Baada ya muda mfupi aliyatoa maisha yake kwa Yesu. Akiwa sasa amejawa
na furaha, alianza kuwaeleza familia na marafiki zake kuhusu imani yake mpya. Hata
hivyo, kulingana na sheria za nchi yake,
Mwislamu anayeacha imani yake ni lazima auawe. Familia ya Abdullah walimkabidhi
kwa mamlaka. Matokeo yake aliwekwa gerezani na kuteswa kwa miezi mingi.
Abdullah alipokataa kumkana Yesu, alipelekwa kwenye
mahakama ya sharia, mahali ambako wahalifu wakubwa kabisa huhukumiwa. Jaji alimwambia
Abdullah, ‘Kana hiyo imani yako mpya nawe utaachiwa huru kabisa. Kama ukikataa,
utakatwa kichwa.’
“Sitamkana Yesu kamwe,” Abdullah alijibu, “Kama mkiniua
nitaenda mbinguni. Lakini damu yangu itakuwa kwenye mikono yenu.” Abdullah alihukumiwa
kukatwa kichwa Ijumaa iliyofuata.
Wakati akingoja siku hiyo ifike, Abdullah alirudishwa gerezani
na akafungwa mikono na miguu. Siku ya kuuawa, hata hivyo, hakuna mtu
aliyetokea! Jumatatu asubuhi iliyofuata walinzi walikuja wakamfungua minyororo
yake na kusema, “Kimbia ewe pepo. Hatutaki kukuona tena!”
Akiwa haamini masikio yake, Abdullah aliomba kuelezwa ni
kwa nini imekuwa hivyo. Walinzi wakamwambia kwamba katika siku ambayo alitakiwa
kuuawa, mtoto wa jaji alikufa ghafla. Matokeo yake jaji alibadilisha ile
hukumu.
Kama ilivyo kwa Wasaudia wengi, Abdullah alitoka kwenye
familia ya kitajiri na alikuwa na kila kitu alichohitaji. Lakini matokeo yake,
si tu kwamba alikataliwa na familia yake, bali sasa alikuwa hana tena kipato. Na
alikuwa hawezi kupata kazi maana alihesabiwa kuwa msaliti. Vyeti vyake vyote alinyang’anywa na angeweza kukamatwa
tena wakati wowote.
Lakini licha ya ugumu wote huo, Abdullah aliendelea kuishi Saudi Arabia kwa miaka
kadhaa huku aliwahubiriwa wengine habari za Yesu.
*******************
Ndugu msomaji, Bwana Yesu yuko kazini Yeye mwenyewe. Sheria
kali za kuwanyima watu uhuru wa kuamua juu ya hatima zao hazitafanikiwa kuzuia
ujumbe wa uzima kuwafikia. Mwanadamu hawezi kamwe kushindana na Muumba wake. Fungua
tu macho na masikio yako. Utashuhudia mengi. Lakini cha muhimu zaidi, mpokee
Yesu awe Bwana na Mwokozi wako sasa.
Ushuhuda huu unapatikana kwa lugha ya Kiingereza hapa.
Waweza kuniandikia maoni yako pia kupitia: ijuekweli77@yahoo.co.uk
Waweza kuniandikia maoni yako pia kupitia: ijuekweli77@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment