Saturday, February 23, 2013

Bwana Yesu Asema na Miryam wa Saudia Kupitia Ndotoni





Ufuatao ni ushuhuda wa dada aitwaye Miryam, kutoka Saudi Arabia, ambaye Bwana Yesu alisema naye kupitia ndotoni. Matokeo yake, dada Miryam alitoka kwenye Uislamu na sasa anamwamini Yesu kama Bwana na Mwokozi wake.


Katika video ya hapo juu, Miryam anahojiwa na mwendeshaji wa kipindi kiitwacho “God of Mracles” au “Mungu wa Miujiza” kinachorushwa na kituo cha TV cha “Jesus Set Me Free”, au “Yesu aliniweka Huru.”


Fuatana na mtangazaji katika mahojiano haya yenye kuonyesha jinsi Bwana Yesu mwenyewe anavyofanya kazi kwenye nchi za Kiarabu ambazo, wao wanadhani kuwa sheria kali zitazuia Injili ya Bwana kupenya. Hawajui kuwa kuta na ngome walizowafungia watu na kuwanyima uhuru zinabomokabomoka na anayezibomoa ni Bwana mwenyewe kwa namna ambao hawana kamwe nguvu ya kuizuia.

Tuesday, February 19, 2013

Maisha ya Wanawake Katika Nchi za Kiislamu





Mwanamke wa Saudia aliyeamua kuumwaga
moyo wake wote


Ni jambo lililo wazi kwamba wanawake katika nchi za Kiislamu wananyanyaswa kupita kiasi. Maisha yao hayana uhuru wala amani kwa kuwa sheria za dini yao zinawakandamiza wao na kuwapendelea wanaume. Hata hivyo, baadhi yao wanatambua hali hiyo na wanapambana kujaribu kuibadilisha. Lakini, ni wazi pia kuwa mapambano yao hayo hayawezi kuwasaidia sana kwa kuwa huko ni sawa na kusema Quran ibadilishwe. Je, hilo linawezekana kwa nchi hizo? Maana tatizo si wanaume au serikali; tatizo ni maagizo ya Mungu wanayemwabudu.


Katika video hiyo hapo juu, tunamwona mwanamke mtangazaji wa kituo kimojawapo cha TV kule Saudi Arabia, akimhoji mwanamke mwingine, Bi. Buthayna Nasser, ambaye naye ni mtangazaji kwenye kituo cha TV. Mahojiano yanahusu mjadala uliokuwamo kati ya wanazuoni wa Saudia juu ya wanawake kuonyesha nyuso zao kwenye TV ya Saudia.

Sunday, February 10, 2013

Baada ya Kuijua Njia ya Kweli, Mwana wa Kiongozi wa Hamas Auacha Uislamu na Kumgeukia Yesu Kristo







Mosab Hassan Yousef ni kijana wa kipekee ambaye ana ushuhuda usio wa kawaida. Baba yake ni mmoja wa waliokuwa viongozi wenye ushawishi mkubwa sana ndani ya kundi la kijeshi la Hamas kule Ukanda wa Magharibi (Palestina). Mosab alikulia kwenye familia iliyoshikilia Uislamu kwa nguvu sana.

Akiwa na umri wa zaidi ya miaka 30 sasa [yaani wakati ushuhuda huu ukiandikwa], ni mshirika wa Kanisa la Kikristo, Barabbas Road kule San Diego, Calif. Aliikana imani yake ya Uislamu, akaiacha familia yake kule Ramallah na anatafuta hifadhi ya kisiasa kule Marekani.

Hadithi ya maisha yake inashangaza sana - uwe unakubaliana au hukubaliani na mtazamo wake. Video ifuatayo inaonyesha mahojiano kati ya Mossab na kituo cha FOX News, akieleza yeye mwenyewe namna Muislamu kutoka Ukanda wa Magharibi alivyogeuka na kuwa Mkristo wa Pwani ya Magharibi.

Friday, February 8, 2013

Kutoka Kwenye Uislamu Hadi Kwenye Ukristo



Jina langu ni Tahir na hii ni safari yangu kutoka kwenye Uislamu hadi kwenye Ukristo.

Mara baada ya kufika Marekani nikitokea Palestina miaka 14 iliyopita, nilimwoa msichana mzuri wa Kikristo. Msichana huyu alijaribu kuwa Mwislamu ili kunifurahisha mimi, lakini kadiri alivyojitahidi kufanya hivyo, ndivyo nilivyozidi kuwa mbali naye. Tulizaa mtoto mmoja, lakini ndoa yetu haikudumu maana ni vigumu sana kupenda wakati moyo wako umejaa chuki. Chuki ndicho kitu ambacho nilifundishwa wakati wa kukua kwangu kule Palestina – chuki dhidi ya Wayahudi, Wakristo na hata dunia nzima. Ukiwa kama Mpalestina, unafundishwa tangu ziku ya kwanza kwamba dunia yote ndiyo inayohusika na mateso yetu, na hasa Wayahudi na Wakristo.

Baada ya kuachana, baadaye mke wangu huyo wa zamani alikuja kuniambia kuwa amembatiza mwanangu. Nilikasirika mno kiasi kwamba nilienda kuingia moja kwa moja kanisani, nikamtukana mchungaji aliyefanya ubatizo ule, na nikamwambia kuwa angeenda jehanamu kwa sababu ya kitendo kile. Sikutaka kabisa mwanangu akue akiwa Mkristo!. Matokeo yake nilipigwa marufuku na mahakama kumtembelea mwanangu maana mke wangu alihofia kuwa ningeweza kuja kumteka mwanangu na kumpeleka Palestina. Hivi sasa sipati nafasi ya kumuona mara kwa mara.

Sunday, February 3, 2013

Muhubiri wa Kiislamu Kutoka Misri Aokoka Baada ya Yesu Kusema Naye Kupitia Ndotoni



Ibrahim alikuwa Mwislamu wa imani kali. Alikuwa mtoa mihadhara katika misikiti mbalimbali nchini Misri. Alikutana na Injili ya Yesu. Moyo wake ulitikiswa. Hakujua amwamini nani – je, ni Yesu au ni Muhammad? Nani angemwambia njia ya kweli ni ipi? Aliinua moyo wake juu mbinguni. “Yehova, nionyeshe njia ya kweli nami nitaifuata kwa gharama yoyote ile,” alisema kwa machozi.

Bwana Yesu mwenyewe alikuja kusema na Ibrahim katika ndoto. Ibrahim aliachana na Uislamu na kumkumbatia Mwokozi. Lakini kundi la Waislamu wenye imani kali la Muslim Brotherhood wangemwacha tu? Vipi kuhusu familia yake?

Kumfuata Kristo kuna gharama. Lakini huwezi kumbadilisha mtu anapomjua Mungu wa kweli ingawaje utampiga, utamfunga, na kumtesa kwa kila namna. Endelea kusoma ushuhuda huu wa kutia moyo na Mungu wa mbinguni atasema na moyo wako kwa njia ya ajabu ambayo itabadilisha kabisa maisha yako....!