Ibilisi akitupwa chini pamoja na majini yake
Kwenye Biblia
katika kitabu cha Isaiah 14:12 tunasoma:
Jinsi
ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi
ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!
Aya
hii inamwongelea Lusifa (ibilisi/shetani) jinsi ambavyo zamani alikuwa juu
lakini akaangushwa chini kwa sababu ya uovu wake.
Kwenye aya hii,
ibilisi anaitwa “nyota ya alfajiri”.
Kwa Kiebrania, jina
hili ni heylel ben shachar.
Waarabu, wao wana
neno hilal, ambalo maana yake ni “mwezi mchanga.”
Na hata Kiswahili
nacho kimechukua neno hilo – “hilali”
Kwa hiyo, tunaweza
kusema kuwa huyu “nyota ya alfajiri”
anaweza pia kuitwa “mwezi mchanga
(mwandamo) mwana wa alfajiri.”
Kwa mujibu wa Isaya
14:12 tuliyoanza nayo hapo juu, tumeona
kuwa aya hiyo inamwongelea ibilisi. Kwa hiyo, huyu “mwezi mchanga
(mwandamo) mwana wa alfajiri” ni Lusifa
au ibilisi mwenyewe.
Ukisogea mbele
kidogo na kusoma Isaya 14:13-14, Isaya anaendelea kumwongelea huyu ibilisi kwa
namna hii:
Nawe
ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka
mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi
juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita
vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye
Aliye juu.
Huyu ibilisi
anataja mambo makubwa mawili:
Moja: Nitapanda
mpaka mbinguni.
Mbili:
Nitafanana nay eye aliye juu.
Kwa hiyo, tangu
zamani ibilisi alitamani kuwa juu ya nyota za mbinguni (nyota hapa ni malaika).
Na lengo lake ni ili afanane na Muumba wake; aogopwe kama Mungu; aabudiwe kama
Mungu.
Na hicho ndicho
kilichosababisha akatupwa nje ya mbingu hadi huku chini.
Ndio maana tunasoma
kwenye kitabu cha Ufunuo 12:7-9
Kulikuwa na
vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye
akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao
hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani,
aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na
malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Lakini je, nia yake
ya kuabudiwa kama Mungu aliiacha?
Ukienda kwenye
Biblia ya lugha yake ya asili (Kiebrania), neno kupanda ni alah.
Ili kuthibitisha
hilo, google: “Strongs Hebrew Greek Dictionary H5927”
Sasa hebu jiulize:
Hili jina liko hapa kwa bahati mbaya?
Je, kwa nini mwezi na nyota huinuliwa juu kwenye
misikiti?
Mat 11:25
Wakati
ule yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa
mambo haya uliwaficha wenye hekima na
akili, ukawafunulia watoto wachanga.
Ndugu yangu, chagua uzima sasa kabla mlango haujafungwa:
Yoh 14:6
Yesu akamwambia, mimi ndimi
njia, na kweli, na uzima; mtu haji
kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
No comments:
Post a Comment