Tuongeee iliyo kweli tu jamani.
Muhammad alipomwoa Khadijah, aliishi
naye kwa miaka zaidi ya 20 bila kuoa mwanamke mwingine.
Maswali yanayokuja akilini ni:
1.
Je, alipenda sana wanawake walio na
umri mkubwa kuliko yeye?
2.
Je, hakupenda ndoa za mitara?
3.
Je, alimheshimu sana au alimwogopa
Khadijah?
Tunapotazama katika Sahih Bukhari Juzuu
3, Kitabu 34, Namba 310 tunaamabiwa kuwa siku moja Muhammad alimwuliza Jarir
ibn Abdullah:
“Have you got
married?"
He replied in the affirmative.
Muhammad then asked, “A virgin or a matron?”
He replied, “I married a matron.”
Then Muhammad said, “Why have you not married a virgin, so that you may play with her and she may play with you?”
He replied in the affirmative.
Muhammad then asked, “A virgin or a matron?”
He replied, “I married a matron.”
Then Muhammad said, “Why have you not married a virgin, so that you may play with her and she may play with you?”
Yaani:
“Umeoa?”
akajibu kwa kukubali.
Kisha Muhammad akamwuliza, “Ni bikira
au mtu mzima?”
Akajibu, “Nimeona mtu mzima.”
Halafu Muhammad akasema, “Kwa nini
hukuoa bikira ili kwamba uweze kuchezacheza na yeye achezecheze na wewe?”
Hii maana yake nini?
Maana yake ni kuwa si kwamba Muhammad
alipenda sana kuishi na Khadijah peke yake. Lazima kulikuwa na sababu zingine
zilizomfanya aishi naye.
Tukichukulia kwamba Muhammad alikuwa
yatima aliyeishi na watu mbalimbali maishani mwake, ni wazi kuwa maisha yake
hayakuwa ya uhakika; na bila shaka, akiwa kama kijana, kama ilivyo kwa binadamu
yeyote, angetamani kupata mahali pa kudumu pa kuishi.
Kwa hiyo, alipompata Khadijah (maana
Khadijah ndiye aliyependekeza waoane), bila shaka Muhammad aliona hiyo kuwa ni
fursa hatimaye ya kupata mahali pa kudumu pa kuishi – tena ukichukulia kuwa
yeye alikuwa maskini na Khadijah alikuwa ni mwanamke tajiri.
Kwa hiyo, tunaweza kabisa kusema kuwa
hakuona mwanamke mwingine kwa sababu yahofu ya kufukuzwa na Khadijah – jambo
ambalo lingemfanya arudi kwenye umaskini wa mwanzo.
Kwa nini tunasema hivyo?
Ni kwa sababu mara tu baada ya Khadijah
kufariki, ilikuwa ni kama geti la gereza limebomoka.
Muhammad aliweza kukusanya wake wengi, na
tunaweza kuamini kabisa kuwa kile ambacho alikuja kumwuliza Jarir ibn Abdullah lazima
kilikuwa moyoni mwake siku nyingi. Kwa hiyo, mauti ya Khadijah ilizalisha fursa
adimu iliyokuwa imetamaniwa na moyo wake
kwa siku nyingi.
Huenda kuna sababu zingine tofauti na
mtazamo wangu.
Nakukaribisha ndugu mwislamu utupe
elimu inayohusu jambo hili.
No comments:
Post a Comment