Wednesday, April 2, 2014

Eti Biblia inataja mashehe, kwa hiyo inaunga mkono Uislamu!
Wahubiri wa ‘injili’ wa Kiislamu wanaendelea kuhaha kuhalalisha quran kupitia Biblia. Nasema ‘kuhaha’ kwa sababu hakika kabisa wana juhudi kubwa mno lakini inasikitisha kwa sababu hakuna hata siku moja waliyowahi kusema jambo lenye ukweli kibiblia linalounga mkono quran kama wasemavyo wao – Mungu ni shahidi yangu. Mara waseme Muhammad ametabiriwa kwenye Biblia; mara waseme Yesu aliposema kuwa ataletwa Msaidizi basi alimaanisha Muhammad, n.k. Ni kituko kimoja baada ya kingine. Na wanayemdanganya ni wao wenyewe pamoja na Wakristo wachache wasiojua Biblia.


Kwa msingi huohuo, wanasema eti Biblia imewataja mashehe; na kwa hiyo kwao huo ni ushahidi kuwa uislamu ulikuwapo tangu zamani.

Acha ninukuu hoja ya mmoja wao kama ilivyo, kuhusiana na suala hili, kisha kama kawaida, utaona jinsi hoja hiyo inavyosambaratika mbele za nuru ya Kristo, yaani neno lake.

Mtu huyu anasema:
Swali kwenu nyinyi ambao hamjabahatika kuwa waislam, yaani Wakristo. Kama uislam uliletwa na muhammad s.a.w, vipi masheikh watajwe ndani ya agano la kale?
Ndivyo walivyosimama mikutano miwili yao walioshukuru nyumbani mwa mungu, na mimi, na nusu ya mashehe pamoja nami.” (Nehemia 12:40)
Mkristo jiulize mwenyewe hili swali; mashehe ni viongozi wa dini ipi? waislam...!? au wakristo?
Mwisho wa kunukuu.

Hapa huyu ndugu wa Kiislamu anaongea kwa ujasiri kabisa na kwa kituo. Na unaona kabisa kuwa moyoni mwake anawaza, “Hapa leo nimewapata Wakristo. Lazima waone kuwa Uislamu ndiyo dini ya kweli.”

Na hivi ndivyo ilivyo kwa hoja zao ZOTE kuhusiana na Ukristo. NI UONGO; NI UONGO; NI UONGO!! NI UPOTOVU MTUPU!!

Na mimi nilimpatia jibu fupi tu na rahisi. Kwanza nikamwambia acha nikupatie maana ya neno ‘shehe’ kutoka kwenye kamusi ya Kiswahili.Kama inavyoonekana hapo juu, kuna maana mbili. Na ni wazi kabisa kuwa, kwa ufahamu wa kawaida kabisa, muktadha wa aya hii ya Nehemia haiongelei maana ya kwanza ya neno hili. Kwanza, wakati Nehemia anaandika, Uislamu haukuwapo. Uislamu ni wa juzijuzi tu; miaka 600 baada ya Yesu kuondoka duniani.

Kisha nikamwambia, soma pia aya hiyo kwa Kiingereza. Imeandikwa hivi: “So stood the two companies of them that gave thanks in the house of God, and I, and the half of THE RULERS with me”

Hilo neno ‘mashehe’ limeandikwa kama ‘rulers’ yaani viongozi. Na hii ndiyo maana inayoendana na ile ya pili kwenye kamusi, yaani wazee wenye busara.

Hitimisho
Usidanganywe na tafsiri za Biblia zinazotolewa na Waislamu (siongelei tafsiri za quran; hilo ni suala jingine). Tafsiri za Biblia zinazotolewa na Waislamu ni uongo na upotoshaji mtupu kwa asilimia 100. Kila wanachosema kuhusu Biblia ni kifungo kinachowapeleka watu kuzimu kama wakikiamini.

Ukiwaamini, utakuwa umetupa taji yako; na umeuza uzaliwa wako wa kwanza kwa ujira wa kunde kama Esau.

Bwana Yesu anasema:
“Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.” (Ufunuo 3:11)


Kaa chonjo; adui anahaha kila mahali kukuibia uzima wako wa milele.

Tafakari

Hoji mambo

Chukua hatua

10 comments:

 1. Ni ukweli mtupu, Yaani kama mtu haijui vizuri bibilia ana danganyika kirahisi sana na waislamu

  ReplyDelete
  Replies
  1. Umesema kweli Nicky. Ndiyo maana hata Bwana alishatuonya kuwa: Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; (1Tim 4:1). Ubarikiwe na Bwana ndugu.

   Delete
 2. Sioni sababu kwa wao kutaka kuihalalisha quran kupitia bible kama quran na neno la mungu kwanini wawe na mashaka mbona wakristo hatuhitaji quran nawala hatuna muda wa kuijadili tumeridhika na ukweli halisi uliomo ndani ya bible

  ReplyDelete
  Replies
  1. Ndiyo kazi ya ibilisi tangu mwanzo. alishajitolea kupindisha Neno la Kweli la Mungu. Hao ni vyombo tu anavyovitumia; na wao wala hawana habari.

   Delete
 3. Kaka jemes, tunazidi kushukuru kwa kazi hii nzuri na iliyojaa utukufu mbele za Mungu; mwenye macho na atazame, na mwenye masikio na asikie kwa makini sauti ya Mungu inayoita ndani yake. Kwa kifupi tu niwashirikishe wengine kwa ambayo nimeona na kusikia kwa masikio yangu wazi wazi kuhusu waislamu. Jana na juzi yaani ijumaa na jumamosi nilikuwa maeneo ya magomeni madaba nafanya shughuli zangu za kujipatia riziki. nilipokuwa nafanya kazi si mbali na ulipo msikiti. na kwa siku mbili hizo walikuwa na mkutano wao wa hadhara na walikuwa watu si wengi sana, ni wa wastani. kama kawaida yao huweka vipaza sauti vinavyosikika mbali . basi mashehe wao wakawa wanasoma koran na kuitia majini; na nakumbuka walikuwa wanawaambia watu hasa wakina mama wa kiislamu pengine na wengine wakristu kuwa wakae chini kwa utulivu maana mahali pale kuna majini na mapepo hivyo wakitembea tembea majini yanaweza kuwakumba alafu ikawa balaaa kwao. yaani wale mashehe walikuwa wanapiga kelele kama vile wananena kwa lugha na baadae nilikuja kuelewa kuwa walikuwa wakifanya hivyo kuitia majini na mapepo yaje mahali pale, na baadae nilisikia mmoja akiamuru mkutano utulie maana majini na mapepo yametanda mahali pele na yapo kwa ajili ya kutatua shida zao, alafu baadae mmoja wao akaanza kutoa ushuhuda huko alikotembelea akitaja morogoro kama mahali mojawapo kuwa watu wengi wamepona na wengine kufanikiwa njia zao kwa msaada wa majini; wakati wote huo nilikuwa nafanya kazi huku nikisali na kukemea maana nilitambua kuwa nilikuwa mahali si salama.

  Nimeona tu nishirikishe hili ili kuweka wazi kuhusu hawa wenzetu kuwa huyo mungu-allah wao wanaomuabudu hakika ni lusifa na si Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo na watu wengi sana wanapotea kwa kukosa maarifa sahihi. Pia ni muhimu kila unapopita ni vema ukamkabidhi Mungu mapito yako maana kwa ibada kama hizo za kuitia majini na mapepo hakika ardhi na njia tuzipitazo zimelaaniwa na zimetanda hizo roho chafu ambao kwa macho ya nyama hatuzioni lakini zipo, ni vema kujihakikishia ulinzi wa Yesu, Roho Mtakatifu kila siku kabla hujatoka nyumbani kwako. Nanyi ndugu zangu waislamu, nawaasa muache kungangania kwenye maangamizi, muokoke, mje kwa Bwana Yesu, yeye aliye kweli na uzima wa milele. lusifa hatawasaidia chochote acheni kujidanganya, majini hawawezi kuwasaidia chochote zaidi sana wanawasafishia njia ya kuelekea motoni.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Shalom shalom Henry. Ni kweli kabisa tunaishi katika nyakati za hatari, hasa yule ambaye hana Yesu kama usemavyo. Biblia inasema katika Isaya 5:14, “Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo.”

   Ibilisi yuko bize sana na maajenti wake na udanganyifu wake ili kuwanasa wanadamu kwa mamilioni. Ni jambo la kushangaza na kusikitisha kuona uongo ambao uko wazi unakubalika!!!

   NI GIZA LA NAMNA GANI HILI KWENYE MIOYO YA WATU? Yaani mtu unaitiwa kwenda kusaidiwa na MAJINI na wewe unaenda kwa utayari wooote kabisa!! Ni ajabu mno mno!!

   Anyway, Biblia inaongelea watu hao kuwa ni: "ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu." (2Kor 4:4)

   Delete
  2. Acheni uongo wenu mnadanganyana wenyewe kwa wenyewe kama tafsir ya mashehe mmebisha sasa angalua traslation ya neno sinagogi nyuma ktk biblia ni msikiti wa wa wayahudi ,swali langu nani anasali msikitini kati ya waislam ma wakiristo?kwa nn mwandisgi asiandike kanisa????

   Delete
 4. Asante kaka James, hakika dunia sasa imechafuka sana, na ndio maaana kila kona ya jiji hili na sehemu mbali mbali nchini utakuta vibao vya waganga wakijinadi kuwa wana uwezo wa kutoa huduma mbali mbali. Hakika tuko nyakati za hatari sana, na najaribu kutafakari kila siku huko tunakoelekea kama miaka hamsini au mia hivi vizazi vyetu vitakuwaje katika mambo ya kiroho? je watakuwepo watakaokuwa wanaabudu katika roho na kweli? au ndo tutakuwa kama ilivyo ulaya kwa sasa? naona pengine kwa sisi waafrika hali itakuwa mbaya zaidi hata pengine kuliko hao wa ulaya/wazungu kwani kwa mwenendo unavyoonekana hali si nzuri. Ni vyema kuliweka hili katika maombi kila mara kaka kwani hakika viko vita vikali sana vya kiroho na shetani anafanya kazi kwa nguvu ya ajabu sana. inasikitisha kuona watu wa Mungu wanapotea namna hii.

  Bwana Yesu na alirehemu taifa letu na dunia nzima kwa hili.

  ReplyDelete
  Replies
  1. na siku hizi hawafichi tena. wanasema wazi. NJOO UPATE PESA ZA MAJINI. NJOO UJIUNGE NA FREEMASSON.

   Ndiyo maana Bwana akasema katika Isaya 5:14, “Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo.”

   LAKINI

   Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia. (Mith 22:3)

   Delete
 5. Yaani we umepotezwa na shetani ,,,ushasikia wapi muislam yeyote hata jina 2 la muislam freemasons zaidi ya majina ya wakiristo,,, yaani shetani amepamba amalili zenu hata hamuoni.sina hata haha ya kutoka andiko kwenye bibilia wala Quran maake sishatolewa nyingi Sana ila kutafakari keeni wakiristo kugumu . Kuna mpaka makanisa yanaitwa masonic church.

  ReplyDelete