Tuesday, March 27, 2018

Muhammad ni "mwana wa uharibifu" (Banu Hashim)



Tena na tena nimekuwa nasisitiza kwamba Mungu wa Biblia SIO mungu wa quran hata kidogo. Ni wawili tofauti.

Mifano ifuatayo inathibitisha hilo:

Mungu wa Biblia anasema: Namtuma Mwanangu KUOKOA ulimwengu
Mungu wa quran anasema: Msiamini hilo. Mungu hana mwana.

…………..
Mungu wa Biblia anasema: Mwanangu ndio mlango PEKEE wa mbinguni.
Mungu wa quran anasema: Msiamini hilo. Matendo mema tu yatosha kukufikisha mbinguni.
 ……………
Mungu wa Biblia anasema: Ili kuwasaidia, nakuja kwenu kama Roho Mtakatifu.
Mungu wa quran na watu wake wanasema: Muhammad ndio Roho Mtakatifu.
…………..
Kama alichosema Yesu ni KWELI, basi alichofanya Muhammad ni:
UHARIBIFU, UHARIBIFU, UHARIBIFU!
UDANGANYIFU! UDANGANYIFU! UDANGANYIFU!

Sasa, katumwa na nani?
Miaka mia nyingi kabla hajaja huyu mpinzani wa Mungu, unabii ulishamtangulia. Mtume Paulo aliongelea kuhusu siku ya Bwana (yaani kurudi kwake Yesu) katika 2 Thesalonike 2:3, akisema:
Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, MWANA WA UHARIBIFU.

“Mwana wa uharibifu” (destroyer) anayetajwa hapa ni “mpinga Kristo”

Kama wewe ni msomaji mzuri wa Biblia, utajua jinsi ambavyo Mungu mara nyingi alituma watu walete ujumbe wake, lakini pia ndani ya majina yao kulikuwa na ujumbe. Kwa mfano:
·      Abrahamu = baba wa mataifa mengi.
·      Adam = anayetoka kwenye udongo
·      Petro = mwamba
·      Danieli = Mungu ni hakimu wangu
·      Habakuki = kumbatia
·      Emanueli = Mungu pamoja nasi
·      Bethlehemu = nyumba ya mikate
·      Yoshua = Yahweh ni wokovu.
Nk

Hata maadui zake, nao amewaseti vilevile waendane sawasawa na kazi zao au na kile wanachokitenda hapa duniani.

Muhammad ametoka katika ukoo wa Banu Hashim, yaani Wana wa Hashim.
Cha kushangaza ni kuwa maana ya jina Hashim ni mharibifu (destroyer).
Kwa hiyo, Muhammad ni MWANA WA MHARIBIFU.

Hivi sasa waislamu wanamsubiri Masihi wao ambaye anaitwa IMAM AL-MAHDI.
Kwa mujibu wa Muhammad, huyu atakuwa ni wa uzao wa 12 wa Muhammad.
Tunasoma kuwa:
Hadhrat Abdullah bin Mas'ood (RA) reports from the Prophet (SAW), who said: "The world will not come to pass until a man from among my family, whose name will be my name, rules over the Arabs."(Tirmidhi Sahih, Vol. 9, P. 74; Abu Dawud, Sahih, Vol. 5, P. 207)

Maana yake ni kuwa:
Hadhrat Abdullah bin Mas'ood (RA) anamnukuu Mtume (SAW), ambaye aliema: “Dunia haitafikia mwisho hadi mtu anayetokea kwenye familia yangu, ambaye jina lake litakuwa ni jina langu, atakapowatawala Waarabu.”

Kwa hiyo huyo naye atakuwa ni MWANA WA MHARIBIFU (uzao wa Banu Hashim)

Biblia inasema kwamba atakuja Mpinga Kristo. Huyu ataanza kwa kujidai kuwa ni mtu wa amani na atasaini mkataba wa amani. Hata Wayahudi nao watadanganyika.
Imeandikwa:
Mtawala huyo atathibitisha agano na watu wengi kwa juma moja. Katikati ya juma hilo atakomesha dhabihu na sadaka. (Danieli 9:27)

Juma moja = siku saba
Siku moja = mwaka mmoja
Siku saba = miaka saba
Katikati = miaka 3 na nusu.

Kwa hiyo, hii ina maana kuwa atatawala kwa muda wa miaka 7.

Na kwa upande wa wenzetu, tunasoma haya:
Abu Sa'id al-Khudari(RA) narrated that the Prophet (SAW) said: Our Mahdi will have a broad forehead and a pointed (prominent) nose. He will fill the earth with justice as it is filled with injustice and tyranny. He will rule for seven years. (Abu Dawud, Sahih, Vol. 2, p. 208; Fusul al-muhimma, p. 275)

Maana yake ni kuwa:
Abu Sa'id al-Khudari(RA) amesimulia kuwa Mtume (SAW) alisema: Mahdi wetu atakuwa na uso mpana na pua iliyochongoka. Ataijaza dunia kwa haki kama ilivyojawa na kukosekana haki na ukandamizaji. Atatawala kwa miaka saba.

Kwa hiyo, huyu ambaye Biblia inambainisha kwamba ni mjumbe wa shetani, kwa wenzetu anaitwa ni mjumbe wa Mungu ambaye wanamngojea kwa shauku kubwa.

Lakini Biblia inaendelea kufafanua juu ya huyu mtu kwamba baada ya miaka 3 na nusu, atavunja mkataba na hapo ndipo uharibifu wake utadhihirika wazi.

Ndugu yangu, chagua hivi leo ni nani utamfuata.
Je, ni Kristo Mwana wa Uzima
au
Ni Mahdi mwana wa uharibifu?

No comments:

Post a Comment