Sunday, June 9, 2013

Akef Tayem, Mwislamu Kutoka Palestina Akutana na Bwana Yesu na Kuokoka – Sehemu ya 3





Mpendwa msomaji na mpenzi wa blog hii, naamini ulishasoma sehemu ya 1 na ya 2 za ushuhuda huu wa Akef. Hii ni sehemu ya 3 na ya mwisho inayoonyesha ukuu, upendo na uweza wa Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, yaani Yesu Kristo. Karibu usome sehemu hii na Bwana Yesu akubariki.

……………………….

Sid Roth:
Ulipomgusa yule mtu aliyekuwa kwenye kiti cha magurudumu, nini kilitokea?

Akef:
Inashangaza. Mimi hata sikuwaza kwamba amngeponywa.  Nilijua ingetokea kwangu. Nilijua kuwa miujiza hutokea kupitia wachungaji lakini si kwa mtu kama mimi. Lakini alikuja mbele akanyosha mkono wake, nami nikamshika.  Na mara aliinuka kutoka kwenye kiti chake cha magurudumu.

Sid Roth:
Kwa nini ulimgusa?

Akef:
Sijui.  Nilijisikia tu shauku aondoke kwenye kiti kile.

Sid Roth:
Alitembea?

Akef:
Ndiyo.  Alianza kwa kunyanyuka polepole, kisha akaanza kutembea mle kanisani. Kisha akatoka nje, akarudi ndani na kila mtu kwenye lile kanisa la Kibaptisti alishangaa. Na kwa namna fulani, kila mtu alitamani kuja mbele na kugusa mkono wangu. Mchungaji alikuja akauangalia mkono wangu – maana uligeuka mwekundu na wenye joto. Aliwaonyesha waumini na kuwaambia waje mbele kuugusa.

Sid Roth:
Pamoja na ukubwa wa muujiza ule, Akef ananiambia kuwa kulikuwako na jambo jingine kubwa zaidi. Lilikuwa ni jambo gani?

Akef:
Lilikuwa ni jambo ambalo lilinifanya nijue ninakosimama; nijue iliko imani yangu. Chuki ambayo nilikuwa nayo dhidi ya Wayahudi; ambayo niliibeba; uzito ule, uliondoka! Uliondoka na kiukweli nilianza kujisikia mzigo moyoni kwa ajili ya Wayahudi. Na nikaanza kuwaza kwamba, kama kuna njia yoyote ya kuwasaidia, basi niko tayari kuwasaidia. Na nilijua kuwa hili ni jambo lililo nje kabisa ya uwezo wangu! Nisingeweza kamwe kufanya hivi! Sasa jambo hili limetokea wapi? Ni nani aliyenibadilisha jinsi nilivyolelewa; kile nilichoamini? Nini kilichotokea? Ni nguvu ya Bwana.

Sid Roth:
Akef, mimi ni Myahudi. Mimi ni Mzayuni. Nina uraia wa aina mbili. Mimi ni Mwisraeli. Ninaamini kuwa watu wangu wana haki na ardhi ya Israeli ambayo Mungu amewaahidia kwenye Biblia yake. Je, unawaza nini juu yangu?

Akef:
Mimi si mjuzi sana wa mambo ya kisiasa …

Sid Roth:
Unawaza nini juu yangu!

Akef:
Ninakupenda! Na nilitamani kukutana na wewe, na nilishakutana nawe muda mrefu uliopita kwenye akili yangu, kwenye moyo wangu. Wewe ni kaka yangu katika Kristo, na kupitia Ibrahimu, baba yetu.

Sid Roth:
Napenda niwaambie (watazamaji) jambo. Kuna machozi yanayotiririka machoni mwangu hivi sasa. Na hili ni jambo lisilo la kawaida linalotokea leo. Huwa halitokei mara nyingi kama ambavyo ningependa, lakini  linanitokea sasa. Na pale linapotokea, ni wakati wa Mungu mimi kukuambia – uwe ni Myahudi, Mwarabu au Mhindu – Mungu ni mkuu sana kuliko yale uliyoambiwa. Mungu ni mwema sana; Mungu ni upendo.

Anakupenda, hataacha kukupenda. Lakini kuna jambo linalokuzuia kupokea utimilifu wa pendo lake. Jambo hilo ni dhambi. Na kama ukimwambia Mungu unatubu dhambi zako … mwambie kuwa unatamani kubadilika lakini hauna nguvu, kisha umwombe nguvu ya kuwekwa huru. Atafanya hivyo. Lakini ni lazima umwendee kwa njia ya Jina pekee ambalo tumepewa wanadamu kwa ajili ya kuokolewa. Jina hilo kwa Kiebrania ni Yeshua, yaani Yesu.

Kama ukisema sala ifuatayo kwa kumaanisha, Mungu atakutakasa, atakufanya upya, atakupa makusudi ya maisha kama alivyofanya kwa Akef. Yeye ni Mungu wa miujiza. Na Yeye ni Mungu wa nafasi ya pili. Omba sala ifuatayo pamoja nami:

Ee Mungu,
Mimi ni mwenye dhambi,
Nimekutenda dhambi Wewe peke yako,
Nami ninatubu.
Ninaamini kuwa damu ya Yesu
Inaniosha dhambi zangu zote,
 Na sasa mimi ni safi.

Na sasa kwa kuwa niko safi,
Ninatamka kwa ujasiri,
Kwamba Yesu ni Masihi wangu na Bwana wangu.

Bwana Yesu,
Karibu ndani yangu,
Tawala maisha yangu,
Uwe Bwana wa maisha yangu.
Katika Jina la Yesu.
Amen.

Sid Roth:
Akef, nikuulize swali moja la harakaharaka. Kwa nini Waislamu hawasomi Agano Jipya, na hasa Injili?

Akef:
Hawasomi Injili kwa kuwa wanaamini kwamba, Mungu, Allah alimpa Yesu Injili. Na wanaamini kuwa Injili ile ambayo Allah alimpatia Yesu, ilipotea.

Sid Roth:
Kwa nini hilo halina ukweli?

Akef:
Halina ukweli kwa kuwa halina mantiki. Hii ni kwa sababu Injili hii ilikuwapo kwenye miaka ya 600 hadi 700 baada ya Kristo. Iweje basi kitabu hiki kipotee tu duniani kote kwa ghafla hivyo? Hakuna aliyewahi kukiona! Yaani vitabu ambavyo viliandikwa maelfu ya miaka kabla ya hapo vipo halafu hiki cha juzi tu ndicho kisiwepo kabisa!!

………………………………….

Ndugu msomaji wa ushuhuda huu, umemsikia au kumsoma Akef.

Tafakari,

Hoji mambo,

Jiulize maswali,

Chukua hatua.

No comments:

Post a Comment