Friday, July 26, 2013

Yesu Aongea na Binti wa Kiislamu; Binti Aokoka





Sharoni hakuwa Mkristo bali alikuwa ni binti wa Kiislamu. Na wala hakuwa amewahi kujifunza habari za Yesu na Ukristo. Lakini Bwana Yesu mwenyewe alimfuata na kujidhihirisha kwake. Je, ilikuwaje, na nini kilitokea baada ya hapo? Tafadhali fuatilia ushuhuda huu wenye nguvu na unaodhihirisha upendo na uweza na uungu wa Bwana Yesu.

Sunday, July 14, 2013

Toufik Alikuwa Mwislamu Lakini Alimwita Yesu, Leo Ameokolewa na Hajawahi Kujuta



Ufuatao ni ushuhuda wa Toufik, ambaye alikuwa ni Mwislamu lakini alikutana na injili ya Bwana Yesu na kubadili welekeo ambao hajaujutia; na hata anapoelezea neema hii ya wokovu wa Yesu aliyoipata, machozi yanamtoka. Pia machozi yanamtoka zaidi anapowafikiria ndugu zake Waislamu ambao wanapambana kwa jitihada nyingi wakijaribu kumpendeza Mungu kwa njia ya matendo yao ya kidini. Toufik analia anapotambua kuwa yote hiyo wanayofanya ni kazi bure kwa kuwa hawajagundua ziri ambayo na yeye, miaka mingi iliyopita, alikuwa hakuijua.

Thursday, July 11, 2013

Kufa kwa Yesu Kristo Maana Yake Nini?




Utakatifu

Mungu ni mtakatifu. Kutenda dhambi ni kukosa utii kwa Mungu. Mungu anasema kwenye Neno lake: Basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu. (Walawi 11:45).

Pia imeandikwa: Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu (1 Petro 1:15).

Kwa kifupi, kuwa mtakatifu maana yake ni kutokuwa na dhambi yoyote. Mungu kamwe hawezi kufumbia macho dhambi hata iwe ni moja. Kamwe! Hafumbii macho hata zile dhambi ambazo sisi tunaziona ni ndogo sana.

Saturday, July 6, 2013

Je, ni Kweli Quran Haijawahi Kubadilika na Wala Haina Mkono wa Mwanadamu Ndani Yake?




Utangulizi
Rafiki yangu Ibra, amekuwa akinishambulia sana kwa kusema kuwa Biblia ni kitabu kisichoaminika bali Quran ndiyo inayopaswa kuaminiwa. Hoja yake kuu, kama ilivyo kwa Waislamu wengine wengi ni kwamba, Biblia imeingizwa maneno ya kibinadamu kiasi kwamba yale ambayo Mungu aliyateremsha ni kama hayapo tena leo.

Katika makala haya ninapenda tuangalie swali kwamba: Je, ni kweli Quran ni kitabu ambacho hakijawahi kubadilika? Je, ujumbe wake ndio uleule ambao aliteremshiwa Muhammad na Allah? Je, ni kitabu cha kuaminika kuliko Biblia kama wanavyosema Waislamu?

Friday, July 5, 2013

Je, Biblia Ina Vitabu Vingapi?




Vitabu 73 au 66?
Leo duniani kuna Biblia yenye vitabu 73 na yenye vitabu 66. Waislamu wamekuwa wakitumia suala hili kama silaha ya kushambulia Biblia kwamba ni kitabu kisichoaminika, wala hakiwezi kumfikisha mtu mbinguni.

Kwa mfano, ndugu yangu Ibra ambaye amekuwa msomaji na mchangiaji mzuri sana wa blog hii ameniuliza kama ifuatavyo:
James, naomba majibu kwa maswali yafuatayo:
-Biblia original kabisa iliyoandikwa na roho mtakatifu ina vitabuvingapi?
-Kitabu cha Danieli kina sura 12 au 14?
-Biblia yenye vitabu 73 na ile ya 66 ipi ya kweli? Je! Hapa kuna mkono wa roho mtakatifu au ubinadamu?
Ukweli unabaki palepale kwamba biblia sio kitabu cha kutegemea sana kwa mambo ya mungu. Hapa duniani biblia ninazojua mimi ziko zaidi ya tano. Na zote zimepishana kwa namba ya vitabu vilivyopo.
Sasa hapo mimi nabaki nashangaa, niamini biblia gani kati ya hizi? Ubabaishaji, kweli haimo.
Tafakari. Jihoji. Kweli imo ndani yako! Soma Qur'ani tukufu.