Monday, November 11, 2013

Urithi wa Uislamu kutoka kwenye dini za kipagani za Uarabuni - sehemu ya 1

Allah alitokea wapi?

Uislamu unajinadi kwamba Allah ndiye Mungu yuleyule aliyejishughulisha ya Wayahudi tokea nyakati za Ibrahimu katika Agano la Kale. Je, jambo hilo ni kweli?

Uislamu ulianza na Muhammad kwenye miaka 600 baada Kristo. Je, kabla yake imani za Waarabu zilikuwaje? Je, yako mambo yoyote kutoka kwenye imani hizo ambayo yaliingia kwenye Uislamu? Kwa maneno mengine, je, Uislamu hauna upagani ndani yake?

Fuatana nami kwenye makala haya marefu yanayochambua chimbuko la Uislamu ili tuweze kuona iwapo upo uhusiano wowote kati ya Uislamu na upagani uliokuwa ukitawala miongoni mwa jamii za Waarabu kabla ya kutokea kwa Muhammad?


Asili Ya Allah

Jamii za wanadamu KOTE duniani zimekuwa na kawaida ya kujiuliza ni wapi ulimwengu huu umetokea, nini maana ya maisha na wapi watu huenda baada ya kufa. Matokeo yake, kila jamii ilifikia kuamini kuwa kuna aliye na nguvu (au walio na nguvu) kuliko wanadamu wote ambao ndio wanapaswa kuabudiwa na kuombwa msaada pale matatizo yanapotokea.

Hawa wenye nguvu wakajulikana kwa majina mbalimbali kwenye jamii tofauti. Vilevile, kila jamii ilianzisha utaratibu maalum wa kuwasiliana na hawa wenye nguvu, yaani miungu.

Lakini jambo moja ni dhahiri, kwamba UKIACHA JAMII YA WAYAHUDI PEKE YAO, jamii zote za wanadamu zilizobakia duniani – iwe ni Afrika, Ulaya, Asia, n.k. - zimeanzia kwenye ibada za kipagani.  Jamii hizi ziliabudu miungu mbalimbali. Na miungu hii iliwakilishwa na vitu kama vile milima, miti mikubwa, jua, mwezi, majoka makubwa, sanamu, wafalme, n.k. Kwa mfano, Warumi walikuwa na miungu kama vile artemi, jupiter, minerva, atlas, n.k. Tazama hapa. Wagiriki walikuwa na miungu kama vile chronos, dionysus, eros, ares, appolo, hermes, poseidon, n.k. Tazama hapa. Wahindi wana miungu kama vile durga, ganesha, garusha, brahma, n.k. Tazama hapa. Imani hizi za kipagani ziliweza hata kukua sana na kuenea maeneo mengi. Kwa mfano, imani ya ubudha ni imani ya kipagani lakini iliweza kuenea sehemu kubwa sana ya Asia – India, Japan, Sri Lanka, Uchina, n.k.

Kwa hiyo, jamii za Kiarabu, kama ilivyo kwa wanadamu wengine, vilevile hazikuwa tofauti. Jamii hizi nazo zilikuwa zina ibada zao za kipagani.

Waarabu walikuwa wakiabudu kile ambacho kinajulikana leo kama “star family”, au “familia ya nyota.” Tazama hapa. Inaitwa ‘familia ya nyota’ kwa sababu walichukulia miungu yao kwa tabia za kibinadamu. Mwezi ulichukuliwa kuwa ni mungu mwanamume na jua kama mke wa mwezi. Kisha hawa walizaa watoto. Kwa mfano, waliaminika kuwa walikuwa na mabinti watatu waliojulikana kwa majina ya al-lat, al-uzza na manat.

Ndiyo maana hata quran ikasema: Have you considered Al-Lat and Al- Uzzah, and another, the third (goddess) Manat? (Sura 53:19-20).

Yaani: Mmemwona Al-Lat na Al – Uzza, na mwingine, wa tatu (mungu mke) Manat?

Na hata Muhammad alikuwa akiabudu miungu hii kabla ya kuanzisha Uislamu. Tunasoma kutoka Hisham al-Kalbi, Kitab al-Asnam (Book of Idols), uk.17 kwamba:


'We have been told that the Apostle of Allah once mentioned al-Uzza saying, "I have offered a white sheep to al-'Uzza, while I was a follower of the religion of my people."

Yaani:
Tulishaambiwa kwamba Mtume wa Allah aliwahi kumtaja al-Uzza akisema, “Nilitoa kondoo mweupe kwa al-Uzza, wakati nilipokuwa nikifuata dini ya watu wangu.” Watu wake ni Waquresh.

Jina Allah linatokana na al-llah. Al ni kama neno la Kiingereza, yaani article ‘a’; na ilah ni mungu. Kwa hiyo, al-ilah maana yake ‘a god’ au tu mungu kwa Kiswahili – maana Kiswahili hakina neno linalofanana na ‘a’.

Kwa sababu lugha huenda ikibadilika, ndipo jina hili likafupishwa na akuwa ‘allah’. Ni kama unavyoona kwenye Kiswahili utasikia mtu akisema ‘mambo ndo ivo bwana.’ Kumbe ‘ndo ivo’ ni kifupi cha ‘ndiyo hivyo’. Huenda miaka hamsini au mia ijayo watu hawatajua kuwa kumbe asili ya ‘ndo ivo’ ni maneno ‘ndiyo hivyo.’

Sasa, allah alikuwa ni nani? Allah alikuwa ni mungu mwezi, ambaye tumesema mke wake alikuwa ni jua na watoto (mabinti zao) walikuwa ni al-lat, al-uzza na manat. Hawa ndio walikuwa wakichukuliwa kuwa ni miungu wakuu miongoni mwa mamia ya miungu iliyokuwa ikiabudiwa na Waarabu kabla ya Uislamu – kipindi ambacho Waislamu hukiita ‘Jahiliyah’.

Na jina hili ‘Allah’ ni jina la kiume (masculine); na ndiyo maana binti yake mmoja akaitwa ‘al-lat’, ambalo ni jina la kike (feminine). Ni kama unavyoona Francis na Fortunatus ni wanaume lakini Francisca na Fortunata ni wanawake – japo majina haya asili yake ni ileile. Ndivyo ilivyo kwa Allah na al- Lat. Yote ni jina lilelile, tofauti tu kwamba moja ni la kiume na jingine la kike.

Mojawapo ya jamii iliyokuwa ikimwabudu sana Allah ilikuwa ni jamii ya Waquresh, ambayo ndiyo jamii alikotokea Muhammad.

Watu wasioelewa wanadhani kuwa Allah alijulikana baada ya Muhammad kutokea. Na wengine nao watasema kuwa Allah alijulikana tangu wakati wa Ibrahimu kama anavyojulikana leo. Kama hilo lingekuwa ni kweli, inabidi wajiulize ilikuwaje Allah wa Ibrahimu akapotea hadi ikawa kwamba kuna Allah wa kipagani?

Mathalani, inafahamika wazi kwamba baba yake Muhammad hakuwa mwislamu bali alikuwa mpagani.

Sitashaangaa endapo baadhi ya Waislamu watasema kuwa baba wa Muhammad alikuwa mwislamu. Hata hivyo, huyu mtu alikufa kabla hata ya Muhammad kuzaliwa. Na je, Muhammad mwenyewe anasema nini kuhusiana na baba yake?

Tunasoma hivi:

Anas reported: Verily, a person said: Messenger of Allah, where is my father? He said: (He) is in the Fire. When he turned away, he (the Holy Prophet) called him and said: Verily my father and your father are in the Fire. (Sahih Muslim, Book 001, Number 0398).

Yaani:
Imeripotiwa na Anas: Hakika, mtu mmoja alisema: Mjumbe wa Allah, baba yangu yuko wapi? Akasema: Yuko motoni. Alipogeka kuondoka, (Mtume mtakatifu) akamwita na kusema: Hakika baba yangu na baba yako wako Motoni.

Na swali ambalo tungependa wajiulize ni kuwa, kwa nini baba yake Muhammad, ambaye alikuwa mpagani aliitwa ‘Abdullah’?

Na kwa kuwa ‘Abdullah’ maana yake ni ‘mtumwa wa Allah’, hii ni ishara ya wazi kwamba wapagani wa kipindi cha jahiliyah walikuwa wakimwabudu Allah hadi kufikia kuwapa watoto wao majina kwa heshima ya Allah – kama ambavyo Wayahudi nao walikuwa wakiwapa watoto wao majina kwa heshima ya Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. 

Kwa mfano:
Yoshua – Yahwe ni wokovu;
Yothamu – Yahwe ni mkamilifu;
Yehoahazi – Yahwe ameshikilia;
Hezekia – Yahwe ametia nguvu;
Elisha – Mungu ni wokovu, n.k.

Jibu liko wazi. Allah alikuwa ni mungu wa kipagani aliyeabudiwa kabla ya Uislamu kuja. Na mungu huyu alikuwa ni ‘mungu mwezi’, yaani ‘al-ilah’. Jina lake jingine aliitwa ‘hubal.’ Mungu huyu wa kipagani aliabudiwa kote mashariki ya kati; wala si kwa Waarabu peke yake.

Hili ni jambo ambalo limeshathibitishwa tena na tena na wanaakiolojia – ambao hufukua masalia ya vitu vya kale – hawa wameshafukua vitu vingi sana ambavyo vinaonyesha jinsi kuabudu mwezi na jua na nyota kulivyokuwa kumeshamiri sana katika eneo la mashariki ya kati.

Na ndiyo maana baba yake Muhammad, yaani Abdullah, alikoswakoswa kuchinjwa na babu wa Muhammad, yaani Abdul Muttalib. Abdul Muttalib  alitaka kumchinja mwanawe huyo kama sadaka kwa Allah. Lakini mjomba wake Abdullah akamwokoa na hatimaye walichinjwa ngamia 100 badala yake. Na ifahamike kwamba machinjo hayo yalifanyikia kwenye kaaba (hili tutaliangalia huko mbeleni).

Tunaambiwa kwamba:
An arrow showed that it was 'Abdullah to be sacrificed. 'Abdul-Muttalib then took the boy to Al-Ka'bah with a razor to slaughter the boy. Quraish, his uncles from Makhzum tribe and his brother Abu Talib, however, tried to dissuade him. They suggested that he summon a she-diviner. She ordered that the divination arrows should be drawn with respect to 'Abdullah as well as ten camels. … the number of the camels (finally) amounted to one hundred. (Ibn Hisham 1/151-155; Rahmat-ul-lil'alameen 2/89, 90).

Maana yake:

Mshale ulionyesha kwamba Abdullah ndiye aliyetakiwa kutolewa kafara. Kwa hiyo, Abdul Muttalib alimchukua yule kijana hadi kwenye Al-Kaaba pamoja na wembe kwa ajili ya kumchinja. Quraish, mjomba wake kutoka kabila la Makhzum na kaka yake Abu Talib, hata hivyo, walijaribu kugeuza mawazo yake. Walipendekeza kwamba amwite mwaguzi wa kike. Huyo aliagiza mishale ya uaguzi ichorwe baina ya Abdullah na ngamia kumi … hatimaye idadi ya ngamia ikafikia mia moja.

Ndiyo maana Mungu wa Biblia alikuwa akiwaonya sana wana wa Israeli juu ya tabia za kipagani za jamii zilizowazunguka kuhusiana na masuala ya kuabudu familia ya nyota au jeshi la mbinguni. Kwa mfano, anasema:

….. tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishiwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo Bwana, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote. (Kumbukumbu la Torati 4:19).


Ikiwa ameonekana katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, upewayo na Bwana, Mungu wako, mtu mume au mke afanyaye yaliyo maovu machoni pa Bwana, Mungu wako, kwa kuvunja maagano yake, …..  naye amekwenda kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyo vyote, nisivyoagiza mimi (Kumbukumbu la Torati 17:2-3).


Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia. (2 Wafalme 21:3).


Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Bwana. (2 Wafalme 21:5).


Akawaondosha wale makuhuni walioabudu sanamu, ambao wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la mbinguni. (2 Wafalme 23:5).nao wataitawanya mbele ya jua, na mwezi, na jeshi lote la mbinguni, walivyovipenda, na kuvitumikia, na kuandamana navyo, na kuvitafuta, na kuviabudu haitakusanywa pamoja tena, wala kuzikwa; itakuwa ni samadi juu ya uso wa nchi. (Yeremia 8:2).

….  na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya dari zake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa. (Yeremia 19:13).


….  na wale walisujudiao jeshi la mbinguni juu ya dari za nyumba; na hao waabuduo, waapao kwa Bwana na kuapa pia kwa Malkamu (Zefania 1:5).

...............................................

Katika mwaka 570 BK, mwaka uleule ambao Muhammad alizaliwa, alikuwapo mtawala mmoja wa dola ya Aksum ya Ethiopia ambaye alikaa Yemen. Huyu aliitwa Abrahah al- Ashram. Inaelezwa kwamba alikuwa na wivu na mji wa Makka kwa jinsi ambavyo watu wengi walikuwa wakienda kuhiji (yaani hija ya kipagani), hivyo na yeye naye akajenga kanisa kubwa kule Sanaa, Yemen akitarajia kuvuta watu wengi, jambo ambalo halikutokea.

Matokeo yake, aliamua kwenda kuvamia Makka kwa lengo la kuiharibu kaaba. Alisafiri na watu wake wengi juu ya kundi kubwa la tembo - ndiyo maana hata mwaka ule ukajulikana kama mwaka wa tembo.

Koo za Kiquresh ziliungana ili kujaribu kuikoa kaaba. Abdul Mutaleb (babu yake Muhammad) aliwaambia watu wakimbilie kujificha milimani wakati yeye na baadhi ya watu walibakia karibu na kaaba. 

Lakini kwa sababu ya ukubwa na nguvu ya jeshi la yule Abrahah, Abdul Mutaleb alisema:


"The Owner of this House is its Defender, and I am sure He will save it from the attack of the adversaries and will not dishonor the servants of His House."
 
Yaani:
Mmiliki wa nyumba hii ndiye atakayekuwa Mlinzi wake, na nina uhakika ataiponya dhidi ya kushambuliwa na maadui na hawatawafedhehesha watumishi wa nyumba yake."  

Mapokeo yanasema kwamba wakati Abrahah anasonga mbele kuiendea kaaba, lilitokea kundi kubwa la ndege ambao walianza kumdondoshea mawe kama mvua hadi wakamjeruhi.  Hivyo, azma yake ya kuiharibu kaaba haikufanikiwa, badala yake akarudi kwake akiwa ameumizwa.

Sasa, swali ni kuwa, kama wakati ule Muhammad alikuwa bado kichanga, na hivyo Uislamu ulikuwa haujaanza; na pale kwenye kaaba inajulikana kwamba kulikuwa na mamia ya miungu ya kipagani; je, Mmiliki wa Nyumba anayetajwa na Abdul Mutaleb ni nani?

Ni wazi kwamba huyu ni mungu wa kipagani, yaani allah aliyekuwa akiabudiwa na kutumikiwa na Abdul Mutaleb, yaani mungu mwezi.

Na swali kubwa zaidi ni kuwa, Quran inasema katika sura Al-Fil (au Tembo) 105:1-5:


"Have you not seen how your Lord dealt with the owners of the Elephant? Did He not make their treacherous plan go astray? And He sent against them birds in flocks, striking them with stones of baked clay, so He rendered them like straw eaten up."


Yaani:


Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo? Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika? Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi, Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni, Akawafanya kama majani yaliyo liwa!

Swali ni kuwa:
Mambo haya yalitokea wakati Uislamu haupo, bali ulikuwa ni wakati wa upagani. Mtumishi wa mungu wa kipagani Abdul Mutaleb alisema kwamba Mmiliki wa Nyumba ile (kaaba) angeitetea.

Je, Mmiliki wa nyumba aliyetajwa na Abdul Mutaleb alikuwa yupi na Mola wako anayetajwa na Quran kwenye sura hii ni yupi? Au tuseme kulikuwa na miungu miwili iliyoshirikiana kumpiga mawe Abrahah na tembo wake? 

Abdul Mutaleb hakumjua Allah wa Muhammad, kwa hiyo kwa namna yoyote ile hangeweza kumtaja huyo (kama kweli Allah wa Muhammad ni tofauti na wa Abdul Mutaleb).

Mazingira yote yanaonyesha kwamba mungu mwezi, aliyeabudiwa na Abdul Mutaleb ndiye aliyeilinda kaaba dhidi ya tembo wa Abrahah. Kwa hiyo, aya hii ya Quran haina uwezo wa kujinadi kwamba inamtaja mungu tofauti na huyo!!


Hitimisho


Kama wewe ni Mwislamu, je, haujiulizi inakuwaje kwamba mwezi ndio wenye usemi juu ya mambo mengi ya muhimu kwenu Waislamu? 

 • Kwa nini ni lazima mwezi uonekane ndipo mfungo uanze? 
 • Kwa nini ni lazima mwezi uonekane ndipo mfungo uishe? 
 • Kwa nini alama kuu juu ya kila msikiti ni nusu mwezi na nyota? Ni nini asili ya vitu hivyo?

28 comments:

 1. Shalom James. Umenifungua kweli. Mungu akubaliki kwa maana nilikuwa najiuliza maswali haya bila majibu. Naomba Roho Mtakatifu azidi kukuongoza na kukuonesha mazito kwa ajili ya utukufu wake. Ubarikiwe sana

  ReplyDelete
 2. Amen. Bwana Yesu akubariki nawe pia Ruta.

  ReplyDelete
 3. Shalom! Nimekuwa nashangaa mungu huyu aitwaye allah alitokea wapi. lakini nashukuru umenifahamisha! ubarikiwe sana!

  ReplyDelete
 4. nikupongeze na nimshukuru Mungu kwa kukutumia na kukufanya ulicho. Mungu akupe afya na uwezo na zaidi.
  si tu waislamu walimodernize upagani hata katoliki kwa sehemu wamefanya hayohayo.
  suala la kuwapa majina watu wanapobatizwa limeagizwa wapi kwenye Biblia, kusheherekea krismasi ni andiko gani limeagiza? yesu alisema tule mwili wake na kunywa damu yake kwa kumkumbuka siyo kumkumbuka kwa kuadhimisha krismasi,toharani(pugratory) sehemu wenye dhambi wanasafishwa kabla ya kwenda mbinguni,kulipa hela ili marehemu asomewe misa.n.k. tumeagiwza kutokuongeza wala kupunguza katika neno la mungu. nje ya Biblia ni kuongeza

  ReplyDelete
 5. Ubarikiwe mtumishi,na jihisi kitu kipya kimeumbika ndani mwangu.

  ReplyDelete
 6. Mungu akubariki mtumishi kwa huu ufafanuzi mzuri

  ReplyDelete
 7. We sema tu una lako jambo na Ukatoliki, endelea kuijua Biblia bila kutimiza yaliyoandikwa uone kama mbingu utaziona na ushangae hao wakatoliki unaowahukumu wanapeta,sisi siyo roboti biblia inayo mageuzi mengi yaliyofanywa na Yesu,we endelea kuikremisha tu.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Mimi sina langu na ukatoliki. Lakini ninalo langu na mafundisho ya uongo wanayodanywa watu - iwe ni wakatoliki wanaodanganya; walutheri; walokole; waislamu, n.k.

   Wanadamu ni mali ya Yesu Kristo; sio wa Ukatoliki. Ukatoliki unadanganya watu wa Mungu aliowanunua kwa damu yake ya thamani. Wana mafundisho mengi ya UONGO. Eneo mojawapo lililosheheni UONGO ni kuhusu bikira Maria.

   Injili ya Yesu ya KWELI ni lazima iwekwe wazi ili Roho Mtakatifu aweze kuwafikia watu wanaodanganywa na walimu wa uongo.

   Nakubaliana nawe juu ya jambo moja. Umesema: [endelea kuijua Biblia bila kutimiza yaliyoandikwa uone kama mbingu utaziona na ushangae hao wakatoliki unaowahukumu wanapeta,]

   Ni kweli. Kama nasema nisiyoyafanya, nitaikosa mbingu. Hilo ni kweli.

   Na wala mimi sisemi kuwa watu hawaendi mbinguni kwa sababu ni wakatoliki.

   Watu hawaendi mbinguni kama wanaishi kinyume na amri za Yesu - wawe wakatoliki au wasiwe wakatoliki.

   Delete
 8. Kwa kweli mtu huyu sina budi kumpongeza kwa mfululizo wa kuendelea kuiendesha kuielekeza na kuendelea kutoa elimu kwa mambo mazuri ya mungu nakupongeza sana sana john endelea kutuelimisha kwan nilikuwa najiuliza mambo mengi juu ya mwezi huu unaofungiwa ukionekana na usipoonekana ni basi la hasha mim bado naendelea kubadilika kupitia blog hii yako asante sana BARIKIWA NA BWANA

  ReplyDelete

 9. Ndugu yangu James, kabla ya kukutajia wenye asili ya Upagani ni akina nani, kwanza kabisa ningependa niondowe uchafu uliyoweka kwa kuusingizia Uislamu kwa kudai eti unatokana na imani ya Kipagani.
  Mimi nadhani wewe James upeo wa uelewa wako ni mdogo sana juu ya Uislamu. Kutokana na fikra asi uliyonae toka ukiwa mdogo, basi unashindwa hata kufanya utafiti wa kina kwa kusoma vizuri vitabu vya mungu ili kubaini pumba na mchele. Badala yake unakuwa na roho ya ukaidi na unakumbatia maagizo ya wanadamu badala ya mungu na huku ukijisifia eti umeokoka na hauna dhambi. Yani wewe kwa jinsi ulivyo na kichwa kigumu hautakubali kamwe kuwa uislamu ndio njia sahihi ya watu wote kuingia mbinguni hata kama Yesu mwenyewe unaemwamini atakuja kukudhihirishia. Lakini mimi nakushauri utumie akili zako katika kutafakari jambo lolote ili likunufaishe. Kumbuka ya kwamba “shina la muhogo mtamu ajua mwenye shamba”. Leo hii sote tunajua ya kwamba, imani zetu zimechimbuka Mashariki ya kati ambako raia wake zaidi ya 90% wameungana na Muhammad (saw). Hii ni ishara tosha ya kukubalika na kwaminika Muhammad. Watu wamesoma vitabu vya kale, wakagagundua ya kwamba kulikuwa na haja ya Mtume wa walimwengu wote kama mungu alivyokaidi. Ndio maana hata wazungu wanamiminikia kwa nguvu zote kwenye dini ya mwenyezi mungu.
  Kwa uzoefu wangu naamini mtu asiyesoma kama Muhammad (saw)hasingeweza kulinganisha maneno na kikapatikana kitabu kizuri kama ilivyo QUR’AN. Naamini angejichanganya na hadi kufikia leo hii, kingeshapotea.
  Ngoja basi nikuelimishe wewe pamoja na mbumbumbu wenzako.
  Ndugu yangu, jina la ALLAH, limetumika kwenye biblia wanayotumia Wakristo wenye asili ya kiarabu, kila mahala penye neno “MUNGU” au “YEHOVA”. Kwa mfano:
  [Mwanzo 1:1 * Biblia ya Kiswahili]"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na na nchi"
  [Mwanzo 1:1 *Biblia ya Kiarabu]"Fiy-al-badi' khalaqa Allahu as-Samawawwat wal Ardh"
  [Yohanna Mt. 3:16 * Biblia ya Kiswahili]"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa..."
  [Yohanna 3:16 * Biblia ya Kiarabu]"Li-annhu haakadha ahabba Allahu ul 'Aalama hataa badhala"
  [Luka 1:30 * Biblia ya Kiswahili]"Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu"
  [Luka 1:30 * Biblia ya Kiarabu]"Laa takhaafiy, yaa Maryam, li-annaki qad wajadt ni'mat(an) 'inda Allahi"
  [Luka 3:38 * Biblia ya Kiswahili]"wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu"
  [Luka 3:38 * Biblia ya Kiarabu]"bni anuusha, bni shiyti, bni Aadama, abni Allahi."

  Kwa mantiki hiyo naona sasa umeamini kwamba ALLAH ndiye Mungu Mwenyezi. Kwa hiyo kama Wapagani wa Kiarabu walitumia hilo jina, kuliitia vitu vyao, basi huo ni ushirikina. Ndio maana Mungu akamtuma Muhammad (saw) kuja kudhihirisha Uislamu kwa yaliyopita, yaliyokawepo, na yajayo pamoja na kubatilisha Ushirikina na kuupa nafasi ufalme wa mbinguni utawale. Hii ni kawaida ya mungu kwamba umtuma mjumbe wake kuja kuwalingania watu, maasi yanapozidi.

  James, WAYAHUDI HAWAJAWA WA KWANZA KUMJUA MUNGU. Huo ni uongo mtakatifu kwa sababu, walikuwepo wachamungu kabla ya WAYAHUDI. Mfano: YAKOBO, ESAU, ISAKA, ISHMAEL, ZIMRANI, YOKSHANI, MEDANI, NA MIDIANI, ISHBAKI NA IBRAHIM, hawakuwa Wayahudi na hata kabla ya Ibrahim walikuwepo pia wachamungu.
  Halafu kitu kama hukijui usikurupuke na kukitolea maamuzi, uliza na utajibiwa. Uislamu haukuletwa na Muhammad (saw). Hata wakati wa Nabii Adam ulikuwepo. Muhammad kaja kwa mwendelezo wa dini ile ile ya Adam, Nuhu, Ibrahim, Ishmaeli, Isaka, Yakobo, Musa, Daudi, Yesu.
  Kwa hiyo ALLAH(sw) wa Muhammad (saw) ni yule yule wa Ibrahim kwa sababu mmoja kati ya watoto wa Ibrahim (Ishmaeli) ni sababu ya kutokea Muhammad (saw).
  Sasa Mungu alimwambiaje Ibrahim? MW17:1
  ITAENDELEA

  ReplyDelete
 10. INAENDELEA
  “Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe MKAMILIFU.”
  Andiko hili Wakristo wengi, hawalijui maana yake. Na kama wangejuwa wasingethubutu kuhubiri utumbo wao wa “IMANI PEKEE BILA YA MATENDO INATOSHA KWENDA MBINGUNI.” Neno hili, mungu analitoa wakati Ibrahim akiwa ni mtu mwenye imani kubwa mbele za Mungu. Lakini mungu akmwambia Ibrahim aende akawe mkamilifu (mnyenyekevu au mtimilifu, au muislam) mbele za mungu kwa kufuata matendo aliyopewa na mungu.

  MW17:7 “Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na UZAO WAKO baada yako, na VIZAZI VYAO, kuwa AGANO LA MILELE, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.”
  Andiko hili, tunapata msingi wa imani ya kweli ya mwenyezi Mungu aliyomfunulia Ibrahim na Ibrahim akawafunulie watoto wake, na watoto wake, akiwemo Ishmaeli, wakawafunulia watoto wao, kizazi kwa kizazi mpaka milele. Upagani ulikuja kama virus kwenye computer. Mungu akamuinstall Muhammad kama antivirus, akafagia ushirikina wote uliokatawala pale Maka na kuiacha imani ya Ibrahim ikirudi kama asili yake. Kwa hiyo wapagani ndio waliokateka jina la ALLAH na ALKAABA na Muhammad akaja kuwapokonya kwa sababu haviwahusu! Hata Yesu aliwakuta watu ndani ya hekalu la Suleiman wakifanya vitu ambavyo havistahili. Akawafukuza na kuiacha nyumba ya mungu kama kawaida. Enzi za Nabii Mussa, Wayahudi walimuasi mungu kwa kutengeneza ndama awe mungu wao.
  Nyota na mwezi juu ya msikiti vinawekwa kwa ajili ya kutambua nyumba ya ibada ya waislamu. Havina husiano wowote na ibada za kislamu. Ndio maana huwezi kuvikuta sehemu nyengine yeyote tafauti na Juu Ya Msikiti. Inasaidia mtu mgeni kutambua kwa haraka msikiti.
  Ila nyinyi wenzetu mnatumia msalaba kila sehemu mnapohusikanapo. Wakati wa kula, kulala, maofisini mwenu, juu ya milima na huku mkijiaminisha kwamba ni alama ya ukombozi kwenu. Na asili ya msalaba ni Upagani.

  AL-KAABA kwa mujibu wa QUR’AN TUKUFU 14:37 imejengwa na Nabii Ibrahim kwa ajili ya ibada. Baada ya miaka tele kupita, washirikina wakaiteka na kufanyia ibada zao.
  Pamoja na washirikina kuiteka ile nyumba ya Mungu, bado hadhi yake ilikuwepo kama nyumba ya mungu, na mmiliki atakuwa mwenyewe mungu kwa sababu hakuna nguvu yeyote yakushindana na Mungu ndio maana akamtuma Muhammad kuja kuirejesha kwa waumini wa kweli na likawezekana kama vile Yesu alipokaikomboa hekalu la Nabii Suleiman mikononi mwa wafanya biashara.
  Sijui wapi unapokwama ndugu James, yani umeshindwa kutumia hakili hata za kwazima kwamba mwezi hauwezi kufanya chochote? Mbona unakufuru wewe Mpagani? Yani kwa akili yako unaipa mamlaka miungu ya kishirikina kwamba ni watendaji kumwaacha mungu mwenyezi?
  Maana yake lile andiko ni kwamba, yeye kama mpagani kajivua. Kamuomba mmiliki wa ile nyumba aiyokoe. Na mmiliki wa nyumba anajulikana kwa mujibu wa hiyo aya hapo juu kuwa ni Mwenyezi mungu.
  Kwa hiyo ndugu yangu, ukiona jambo lolote linatendeka,hapana mwingine ila Mwenyezi Mungu pekee.
  ITAENDELEA

  ReplyDelete
 11. INAENDELEA

  SASA WAPAGANI NI AKINA NANI?
  JIBU: NI WAKRISTO!
  KWA SABABU GANI?
  JIBU: IBADA ZAO NI TOFAUTI KABISA KAMA ALIVYOFUNDISHA YESU.
  ANGALIA HAPA:http://www.paganchristianity.org/pc.pdf
  MPAGANI anadai yeye anapolisujidia sanamu, anatambua ya kwamba lile ni sanamu tu na wala sio mungu. Ila roho wa mungu anashuka kwenye hilo sanamu na kumfanya yeye amwabudu mungu wake kupitia sanamu.
  MKRISTO anadai Yesu ni mwanadamu ila roho wa mungu yuko juu yake na hivyo anakuwa mungu.
  Mpagani na Mkristo wameachana nini?

  Yesu, aliwahi kuwafundisha wanafunzi jinsi ya kusali, akaanza hivi: Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe....
  Sasa nyinyi Wakristo mnapoanza tu lazima mtumbukize: kwa jina la baba na la mwana na la roho mtakatifu. Mmepata wapi fundisho hili?

  Papa Benediktine XVI alisema hivi: The christianity is not a religion of the book. A man made. Yaani: ukristo sio dini ya kwenye kitabu. Umetengenezwa na mtu tu.( kwa maana nyengine hauna baraka za mungu). Je, ni kweli au uongo? Kama ni uongo, naomba ushahidi nipatiwe.

  WALOKOLE mnadai kwamba WAKATOLIKI ibada zao ni za kipagani, Yesu alisema atakuja roho wa kweli kuwasaidia ili muwe katika kweli, VITABU VYOTE VYA INJILI, vimekusanywa na WAKATOLIKI, baada ya kuonekana vitabu vingi, wao wakachagua baadhi, ambavyo ndio hivi vinavyotengeneza injili inayoaminika leo hii.
  Swali: kwa kuwa vitu vyote vya kidini vilifanyika huku vikiongozwa na roho mtakatifu na nyinyi walokole mnawatuhumu wakatoliki, ikiwa na maana, wakatoliki hawakuongozwa na roho mtakatifu, ndio maana walikuwa wanaenda kinyume na maadili ya dini na vitabu vya injili wamechagua wao na vingine kuvichoma moto. Je kuna haja ya kuiamini injili kwamba imetimia?

  ReplyDelete
 12. Ibrabura add me please,ni wewe ndiye uliyenipunguzia jazba kwa huyu jamaa anayejifanya kumjua ALLAH za yetu waislam,jazaakallaahu kheir! Facebook natumia jina la Mume Wa Leylah Marius

  ReplyDelete
  Replies
  1. pole kwa maumivu ya jazba. sasa si uje kwa Yesu uondokane na utumwa huo?

   Delete
 13. ibrabura umeeleweka sana. unajua hawa ndugu zetu wanajitahidi sana kutafuta kasoro ndani ya uislamu lakini naamini hawatapata abadani. Quran haikuchakachuliwa, ni halisi tangu Enzi na Enzi hata mitume wakifufuka leo hawataona kasoro yoyote katika quran, lakini katika biblia kwanza watajiuliza hiki kitabu kinachofanana na biblia kinatoka wapi. yaani haitakuwa biblia bali itafananishwa na biblia kwasababu tu ya baadhi ya mistari michache ambayo haikubadilishwa.

  ReplyDelete
 14. We love you so much brother James

  ReplyDelete
 15. We can't pay you Mr Jame lakini tunaweza kuomba Mungu akubariki.Have all blessings in Mighty Name of Jesus.

  ReplyDelete
 16. Kabla ya yote wacha nikushukuru brother Jame kwa kazi nzuri saana,Mungu akubariki.Mr ibrabura na wezako wale wako na imani kama yako;Ati unasema sisi Christian tulitoka kwa imani ya Catholic kwa sababu dio walikuwa wa kwanza ama wao dio walitoa Bible?.. Kitu unastahili kujua nyuma yako haina maana kama hapo upo na bale unaenda.Kama wazazi wako walikuzaa wakiwa maskini sasa unataka kumanisha nienderee kuwa maskini? Ama nitoke kwa mamangu nitafute wazazi mwenye wako na Pesa dio Nisiwe maskini? Hapana! Ninastahili kusoma kwa bidii ili nikipata pesa wakae na Maisha poa...Ata kama tulianzia na catholic(maskini),jua tuko na Mwalimu(Roho mtakatifu) alitufunza sasa tuko sonko(wokovu)..
  Kuna Mwislamu siku Moja aliniabia ati Adam alikuwa Mwislamu,;Kwanza unajua ni kwa nini Abraham alitolewa kwa babake? Ebu soma "Yoshua akawaambia watu wote, BWANA, Mungu wa Israel, alisema hivi,Baba zenu hapo zamani walikaa ng'ambo ya Mto,Maana Tera,Baba yake ibrahimu, naye ni Baba yake Nohori; wakaitumikia miungu mingine." (Yoshua 24:2)
  Arafu hapo juu Mr ibrabura unasema ati ata Ishmaeli ni wa agano la Mungu kwa uzao wa Ibrahimu? Ebu soma "Mungu akasema, Sivyo, Lakini, Sara mkeo atakuzalia MWANA wakiume nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano LA milele kwa ajili ya uzao wake baada yake. Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia,nimembariki,nitamzindisha, nami nitamwongeza sana sana, Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitafanya awe taifa kuu" (Genesis 17:19-20)
  Wacha kutoa kitu kwa kichwa toa kwa Neno LA Mungu na liko wazi kila mtu.

  ReplyDelete
 17. Mungu akubariki sana Kaka kwa uandishi wenye FACTS na ULIOTUKUKA.

  ReplyDelete
 18. Wanasema Mtume wa mwisho ni Muhammad, halafu Yesu sio Mungu ni Mtume ok fine sasa atakaporudi atarudi na title ipi na wa mwisho alishafunga ukurasa Mohamad. Kama Yesu atarudi how comes Muhamad awe wa mwisho. Na kwa nini aje amuhukumu Dajal (Ibilisi) na yeye ni nabii tu? Hamumuogopi hata kwa mamlaka hayo makubwa aliyonayo

  ReplyDelete
  Replies
  1. Uko sahihi sana Hemedi. Kwa yeyote anayeamua kufungua macho yake na kutazama KILA KITU kinachotajwa na maandiko kuhusu Yesu, lazima atatambua ukuu na uungu wake. Lakini kwa yule anayechambua ayatakayo na kufumbia macho asiyoyataka, lazima atandanganyika.

   Delete