Kwenye
facebook kuna hoja nyingi zinazozungumziwa humo. Nikakutana na ndugu mmoja mwislamu anatoa
hoja kwamba Yesu amelaaniwa, hivyo hana uwezo wa kuokoa mtu. Na anatoa kabisa
maandiko ya Biblia, eti kuthibitisha hoja zake - si kwa kudhihaki, bali kwa kuamini kabisa kwamba hivyo ndivyo ilivyo! Na hivi ndivyo hali ilivyo
kabisa kwa Waislamu linapokuja suala la kutafuta sababu za wao kuukataa wokovu
wa Yesu Kristo.
Basi nilianza kujibu hoja za ndugu huyu. Na sasa, kwenye makala haya, nitanukuu vilevile majibizano yetu yalivyokuwa ili iwe ni msaada kwa wengine, maana ni wengi walio kama yeye.
Basi nilianza kujibu hoja za ndugu huyu. Na sasa, kwenye makala haya, nitanukuu vilevile majibizano yetu yalivyokuwa ili iwe ni msaada kwa wengine, maana ni wengi walio kama yeye.
Nafikiri
si vibaya mtu kujenga hoja ili kukataa au kukubaliana na jambo fulani. Lakini
kinachosikitisha ni kujenga hoja juu ya msingi wa uongo! Ni sawa na mimi nianze
kusema kuwa simwamini Muhammad kwa sababu alikuwa alifundisha Uislamu lakini
yeye alikuwa Mkristo. Hii ni hoja ya uongo kabisa. Muhammad hajawahi kuwa
Mkristo. Kama ninataka kutoa hoja ya kutomwamini Muhammad, nitatafuta hoja ya yenye ukweli –
kama ipo; lakini si kusimamia kwenye hoja ya uongo! Nitakuwa najidanganya mwenyewe!!
Basi hivi ndivyo majibizano yetu yalivyokuwa na huyo ndugu mwislamu:
Basi hivi ndivyo majibizano yetu yalivyokuwa na huyo ndugu mwislamu:
YEYE:
Hawezi kuokoa mtu aliyelaaniwa,GALATIA 3:13. Kwa mujibu wa andiko hilo Yesu
amelaaniwa na Mungu. Vipi mwenye laana aweze kuokoa watu? Nendeni mkaihubiri
injili kwa kila kiumbe. Nami ni kiumbe nataka kufundishwa Injili na nyie
mnayoijua Biblia; Galatia 3:13 na Kumbukumbu la taurati 21:22 maandiko hayo
yanamaanisha niniiii?
[Sijui ndugu msomaji kama unaona jinsi anavyoingiza hoja yake hii kwa ujasiri na kujiamini kabisa? Yaani ana UHAKIKA kwamba nikiwaambia Wakristo walete maana ya maandiko haya, watakwama tu. Hivyo, wataona jinsi ambavyo wamepotea; na yamkini wataukubali Uislamu. Hapa hatanii. Anaongea kwa nia njema kabisa akiamini kuwa yuko sahihi. Na sababu ya ujasiri wa ndugu huyu ni kwa sababu Wagalatia 3:13 inasema: Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa ALIFANYWA LAANA kwa ajili yetu; maana imeandikwa, AMELAANIWA KILA MTU AANGIKWAYE JUU YA MTI.
Na Kumbukumbu 21:22 nayo
inasema: Ikiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa, akauawa, nawe ukamtundika juu
ya mti; mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti; lazima utamzika siku iyo
hiyo; kwani aliyetundikwa AMELAANIWA NA MUNGU; usije ukatia unajisi
katika nchi yako …
MIMI:
Rafiki, maana yake uache kung'ang'ana na kupambana na kujikosha mwenyewe kwa
kudhani utakuwa mtakatifu kwa jitihada zako, bali ukubaliane na ukweli kwamba
Yesu alikupenda tangu kale, akaja akatundikwa msalabani, si kwa dhambi zake
(maana hakuwa na dhambi), bali ni kwa dhambi zako na zangu. Yeye alijitoa
sadaka ili KWA IMANI TU uweze kusamehewa dhambi zako unapotubu kwa JINA LA
YESU. Vinginevyo kama utaendelea kujitahidi kutenda matendo yale uliyoambiwa
kuwa ni mema ili kwamba eti ndio yakuwezeshe kwenda mbinguni, basi jua kwamba
mbingu umeshaikosa tayari.
YEYE:
Sawa sawa kwa kuwa Yesu alilaaniwa kwa dhambi zenu.Yeye Yesu atakwenda wapi?
Ndugu
zangu tuacheni ushabiki katika dini. Dini si ushabiki someni na waulizeni
wachungaji wenu maswali msikubali kufundishwa bila ya kuuliza maswali. Naiusia
nafsi yangu na kuwausia ndugu zangu katika ADAM, Yeyote atakayekufa hali ya
kuwa ni Mkristo atakwenda motoni. Si maneno yangu bali ya Biblia. 1Wakorintho
15:18. Anayebisha na akafute andiko hilo!
[Sijui ndugu msomaji kama
unaendelea kuona nia ya dhati iliyo ndani ya ndugu huyu Mwislamu ya kutaka watu
waifahamu ile anayodhani yeye kuwa ndiyo KWELI? Huyu ndugu si kwamba ni mwabudu
shetani anayetaka kuwatega Wakristo na watu wengine ili awanase na kuwapeleka
kwa shetani; hapaha! Ni mtu ambaye anaamini kabisa kwamba yuko kwenye njia
sahihi ya kwenda mbinguni. Unakuja tu kugundua shida kubwa kwenye misingi ya
hoja zake. Anatoa maandiko kwa ujasiri kabisa akiamini yanasapoti kile
anachokiamini, kumbe wala hayamuungi mkono hata kidogo. Hoja zake zimejengwa kwenye
msingi wa UONGO kama nilivyotangulia kusema. Kwa hiyo, hata kama nia yake ni
njema, huo msingi wa uongo ndio uangamivu wake – huo ndio utakaomwangamiza. Mara
nyingi huwa natoa mfano kwamba, kama una kiu na ukakuta kuna kimiminika fulani
kama maji kiko kwenye kikombe nawe ukakinywa, japo nia yako ilikuwa ni njema,
yaani kukata kiu, kama kile kimiminika ni sumu, utakufa tu! Nia njema si
garantii ya usalama wako; bali ni nia njema pamoja na maarifa sahihi. Yaani, nia
njema pamoja na kweli. Basi tukaendelea kujibizana na ndugu huyu.]
MIMI: Rafiki, mbona Waislamu huwa mnatoa
reference za ajabuajabu sana. Mwenzako mwingine aliambiwa na ustaadhi wake kuwa
Biblia inamwongelea mkuu wa ulimwengu. Akaambiwa kuwa mkuu wa ulimwengu ni Muhammad. Kwa
hiyo, Biblia imemtaja Muhammad. Alipofunuliwa
andiko hilo kwenye Biblia na mchungaji mmoja siku moja, akakuta kumbe Biblia
inamaanisha ni shetani. Alifedheheka sana. Sasa na wewe unatoa 1 Wakorintho
15:18 kwa ujasiri kabisa. Inasema hivi: Na hapo wao nao waliolala katika Kristo
wamepotea. Ulipoona hivyo ukajua, Ehe! Wakristo wamepatikana. Mkasahau kwamba
mstari wa 16 unaanza hivi: MAANA KAMA WAFU HAWAFUFULIWI ..... Kwa maana
nyingine, kama wafu hawafufuliwi basi ndipo mstari wa 18 unaleta maana hiyo
mnayoitamani sana iwe kweli. Njoo kwa Yesu acha ukaidi na ubishi.
Pia,
unauliza, kwa kuwa Yesu alilaaniwa kwa dhambi zetu atakwenda wapi? [alilaaniwa na
kwa dhambi zako pia]. Mwanao akiiba kisha mahakama ikaamuru alipe faini ya laki
moja au aende jela, wewe hutalipa faini hiyo? Je, ukilipa inakuwa sadaka au
bado ni faini? Je, unapolipa wewe unageuka kuwa mhalifu? Lakini mwanao huyo
akikataa malipo yako mahakama itamwachia? Wewe na mimi ni watenda dhambi na
sheria ya Mungu ilishatuhukumu kwenda jehanamu milele. Yesu ni Baba aliyekuja
kulipa faini. Wote walioamini juu ya kazi hiyo ya upendo, Mungu anawaacha huru.
Wote wanaosema 'sina haja na faini aliyolipa Yesu' wanabakia na hukumu yao na
jehanamu inawangoja bila shaka. Kwa hiyo, jibu lako liko wazi sana: Mlipa faini
ya mkosaji huwa hageuki kuwa mhalifu!! Njoo kwa Yesu leo.
YEYE:
Hayo ni maneno yako si maandiko. Mimi nataka maandiko,"Aliye laaniwa
anakwenda wapi? Kwa imani zenu Galatia 3:13 & Kumbukumbu la taurati 21:22
Yesu alifanywa laana kwa dhambi zenu kwa kuwa sijaona andiko la yeye kusamehewa
baada ya kuchukua dhambi zenu. Je yeye atakwenda wapi? Na kama kuna andiko la
yeye kusamehewa dhambi alizochukua kutoka kwenu naomba unitajie!
[Unamwona
tena ndugu huyu. Yaani anajiamini kwelikweli! Unajua, mtu hawezi kujiamini
kiasi hiki kama anajua kabisa kwamba amekosea. Lakini kama moyo wake unamwambia
kuwa YUKO SAHIHI KABISA, anakuwa na ujasiri mkubwa sana – hata kama hayuko
sahihi! Na kama nilivyoanza na mfano mwanzo wa makala haya, maamuzi YOTE ya mtu
kama huyu kuhusiana na Yesu na Ukristo, yanakuwa yanatokana na hiki ambacho
kimo ndani yake – bila kujali kina ukweli au hakina ukweli. Hakika kabisa, Mungu ni shahidi wangu, hii ndiyo hali ya ndugu
zetu Waislamu! Inasikitisha! Basi tukaendelea kuhojiana.]
MIMI:
Ndugu, unataka maandiko. Mbona yapo mengi tu.
Rafiki, dhambi haitoki mwilini; inatoka moyoni. Kumbuka hilo. Ndiyo maana dhambi haioshwi kwa maji! Bwana Yesu aliye Mwalimu Mkuu anasema: Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni? BALI VITOKAVYO KINYWANI VYATOKA MOYONI; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi. Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano HAYO NDIYO YAMTIAYO MTU UNAJISI…. (Mt 15:17-20).
Rafiki, dhambi haitoki mwilini; inatoka moyoni. Kumbuka hilo. Ndiyo maana dhambi haioshwi kwa maji! Bwana Yesu aliye Mwalimu Mkuu anasema: Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni? BALI VITOKAVYO KINYWANI VYATOKA MOYONI; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi. Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano HAYO NDIYO YAMTIAYO MTU UNAJISI…. (Mt 15:17-20).
Yesu hakuwahi kutenda dhambi. Maandiko matakatifu yanasema wazi: YEYE ASIYEJUA DHAMBI ALIMFANYA KUWA DHAMBI KWA AJILI YETU, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye. (2 Wakor 5:21).
Sasa kwa nini alihesabiwa kuwa mwenye laana? Imeandikwa: Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe KATIKA MFANO WA MWILI ULIO WA DHAMBI, na kwa sababu ya dhambi, ALIIHUKUMU DHAMBI KATIKA MWILI (Warumi 8:3).
Mwili wake ndio uliopata adhabu. Sasa wewe unauliza kwamba, “Sasa yuko wapi?” Na mimi nikuulize, baada ya kufa kinachoendelea huko mbele ya safari huwa ni mwili au huwa ni roho?
Naamini unafahamu kuwa kinachoendelea na safari ng’ambo ya mauti ni roho. Na kwa kuwa roho ya Yesu haijawahi kutenda dhambi, unadhani yuko jehanamu au yuko mbinguni? Kama unadhani yuko jehanamu, ataendaje huko wakati hana dhambi?
Maandiko yanasema:
roho ile itendayo dhambi itakufa. (Ezekiel 18:4). Sijui kama unaona kuwa katika
andiko hili anaongelea roho kufa; si mwili? Kufa kwa roho maana yake kutupwa
jehanamu ya milele na Mungu kwa sababu ya dhambi. Sasa, roho ya Yesu haikuwahi
kutenda dhambi. Je, bado unadhani iko jehanamu?
Kwa kuhitimisha,
Biblia inasema hivi: Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya
dhambi, MWENYE HAKI KWA AJILI YAO WASIO HAKI, ili atulete kwa Mungu; MWILI WAKE
AKAUAWA, BALI ROHO YAKE AKAHUISHWA (1 Petro 3:18).
Ndugu, ukimkataa Yesu kama sadaka ya dhambi zako, unabaki na dhambi hizo kwa maana kila roho ya mwanadamu ina dhambi. Kwa hiyo, njia ya kwenda mbinguni imefungwa kwako (kimsingi umejifungia mwenyewe); bali njia ya kwenda kuzimu iko wazi kwako (ambayo umejifungulia mwenyewe)! Uamuzi ni wako. Chagua uzima ulio katika Kristo Yesu ili upone.
………………………………………………
Sijamsikia
tena ndugu huyu baada ya kumpa jibu hili. Sijui kama bado anajipanga au
ameshaelewa ukweli wa mambo. Lakini ninachotaka kusema ndugu zangu Waislamu,
hakuna ubaya kujenga msimamo juu ya maisha yako na yale mambo unayoyaamini.
Lakini swali la msingi ni kwamba, “Je, umejenga falsafa ya maisha yako na imani
yako juu ya msingi sahihi? Yale uliyoambiwa kuhusiana na Ukristo, Yesu na
wokovu wake yametokana na maneno ya kweli? Kupinga Ukristo, hata ukifanya hivyo
kwa nguvu zako zote; hadi ukatoa na uhai wako kwa jambo hilo, swali linabaki
palepale, je, msingi wako ulikuwa umejengwa kwenye KWELI? Au ulikuwa tu
unatumiwa na watu kwa ajili ya maslahi yao wenyewe?
Yapo
mafundisho mengi, mengi, mengi mno mnayofundishwa Waislamu kuhusiana na Ukristo
ambayo ni UONGO mtupu. Lakini hayohayo ndiyo yamekuwa MSINGI ambao juu yake
mmejenga imani yenu na hoja zenu kwa nini hamtaki kuamini kuwa Yesu Kristo ni
Mwokozi wa ulimwengu wote; na kwamba bila Yeye, hakuna hata mwanadamu mmoja
atakayeingia mbinguni!
Tafakari
Chunguza mambo
Hoji
Chukua hatua
ndugu yangu, biblia huwa inajitafsir yenyewe, tatizo lenu wakristo mnalazimisha ili maana za biblia ziendane na zenu.
ReplyDeleteAsante sana brother Oscar kwa kuitikia makala haya. Mimi ni binadamu siwezi kujisifu kuwa najua kila kitu. Ni kweli kabisa kuna mambo mengi SANA katika Biblia ambayo sijayafahamu; na pia mengi sitayafahamu hadi naondoka kwenye dunia hii.
DeleteSasa, kuhusiana na makala haya, je, ni kitu gani humu ndani ambacho unadhani kimetafsiriwa kinyume na Biblia inavyojitafsiri?
angalia council of nicea ndio msingi wa ukristo ulipoanza ndipo yesu alipewa uungu
DeleteBARAKA NA AMANI YAKE MUNGU WETU IWE PAMOJA NANYI WOTE MTAKAO SOMA UJUMBE UHU. BIBLIA IPO WAZI SANA KWA WALE WALIO JALIWA NEEMA YAKULIKUBALI NENO LA MUNGU NA NDO WALE WANAO LIELEWA. KUNA WATU WENGI WANAO MZUNGUMZIA YESU KWA NJIA YA MWILI...SASA WEWE KAMA MKRISTO UNAPO MFUNDISHA YESU KWANJIA YA ROHO LAZIMA KUWEPO NA UTATA SABABU WAMEPFUSWA MACHO HAYAHONI.
ReplyDeleteamen. Baraka na amani ziwe nawe pia ndugu yetu.
DeleteNo need to worry, wewe fanya dhambi zako jc alishazibeba yani kama ni mwezi poa, kama kahaba endelea, kama muongo usiache
ReplyDeletehaleluyah
hahaaaa,wakristo imani yenu haieleweki,kuabudu kwenu ni kupiga ngoma na mziki..wapi na wapi hayo?
ReplyDeleteNajifunza mengi sana tuu asee.
ReplyDeletewapi andiko YESU ALIFUTIWA LAANA ALOIPATA BAADA ya KUTUNDIKWA MSALABANI ndo awe hataingia MOTONI???
ReplyDeleteyesu hakuwa na dhambi?
ReplyDeleteila alitundikwa msalabni na hivo kulaaniwa?
maana awekwae kwenye mti amelaaniwa na mungu?
wapi aya yesu amesafishwa dhambi ili awe msaafi kupokelewa?
msaada hapo!!!
alafu biblia inadai kuwa kila mtu atabeba mzigo wake (dhambi)
ikiwa wewe umezaliwa juzi juzi tu hapa..
je Furushi gani la kwako alilobeba ikiwa yeye kashabeba ya nyuma?