Tuesday, January 14, 2014

Eti Yesu Amelaaniwa Hawezi Kuokoa




Kwenye facebook kuna hoja nyingi zinazozungumziwa humo. Nikakutana na ndugu mmoja mwislamu anatoa hoja kwamba Yesu amelaaniwa, hivyo hana uwezo wa kuokoa mtu. Na anatoa kabisa maandiko ya Biblia, eti kuthibitisha hoja zake - si kwa kudhihaki, bali kwa kuamini kabisa kwamba hivyo ndivyo ilivyo! Na hivi ndivyo hali ilivyo kabisa kwa Waislamu linapokuja suala la kutafuta sababu za wao kuukataa wokovu wa Yesu Kristo.
 

Basi nilianza kujibu hoja za ndugu huyu. Na sasa, kwenye makala haya, nitanukuu vilevile majibizano yetu yalivyokuwa ili iwe ni msaada kwa wengine, maana ni wengi walio kama yeye.


Nafikiri si vibaya mtu kujenga hoja ili kukataa au kukubaliana na jambo fulani. Lakini kinachosikitisha ni kujenga hoja juu ya msingi wa uongo! Ni sawa na mimi nianze kusema kuwa simwamini Muhammad kwa sababu alikuwa alifundisha Uislamu lakini yeye alikuwa Mkristo. Hii ni hoja ya uongo kabisa. Muhammad hajawahi kuwa Mkristo. Kama ninataka kutoa hoja ya kutomwamini Muhammad, nitatafuta hoja ya yenye ukweli – kama ipo; lakini si kusimamia kwenye hoja ya uongo! Nitakuwa najidanganya mwenyewe!!

Basi hivi ndivyo majibizano yetu yalivyokuwa na huyo ndugu mwislamu:


YEYE: Hawezi kuokoa mtu aliyelaaniwa,GALATIA 3:13. Kwa mujibu wa andiko hilo Yesu amelaaniwa na Mungu. Vipi mwenye laana aweze kuokoa watu? Nendeni mkaihubiri injili kwa kila kiumbe. Nami ni kiumbe nataka kufundishwa Injili na nyie mnayoijua Biblia; Galatia 3:13 na Kumbukumbu la taurati 21:22 maandiko hayo yanamaanisha niniiii?

[Sijui ndugu msomaji kama unaona jinsi anavyoingiza hoja yake hii kwa ujasiri na kujiamini kabisa? Yaani ana UHAKIKA kwamba nikiwaambia Wakristo walete maana ya maandiko haya, watakwama tu. Hivyo, wataona jinsi ambavyo wamepotea; na yamkini wataukubali Uislamu. Hapa hatanii. Anaongea kwa nia njema kabisa akiamini kuwa yuko sahihi. Na sababu ya ujasiri wa ndugu huyu ni kwa sababu Wagalatia 3:13 inasema: Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa ALIFANYWA LAANA kwa ajili yetu; maana imeandikwa, AMELAANIWA KILA MTU AANGIKWAYE JUU YA MTI.

Na Kumbukumbu 21:22 nayo inasema: Ikiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa, akauawa, nawe ukamtundika juu ya mti; mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti; lazima utamzika siku iyo hiyo; kwani aliyetundikwa AMELAANIWA NA MUNGU; usije ukatia unajisi katika nchi yako …

MIMI: Rafiki, maana yake uache kung'ang'ana na kupambana na kujikosha mwenyewe kwa kudhani utakuwa mtakatifu kwa jitihada zako, bali ukubaliane na ukweli kwamba Yesu alikupenda tangu kale, akaja akatundikwa msalabani, si kwa dhambi zake (maana hakuwa na dhambi), bali ni kwa dhambi zako na zangu. Yeye alijitoa sadaka ili KWA IMANI TU uweze kusamehewa dhambi zako unapotubu kwa JINA LA YESU. Vinginevyo kama utaendelea kujitahidi kutenda matendo yale uliyoambiwa kuwa ni mema ili kwamba eti ndio yakuwezeshe kwenda mbinguni, basi jua kwamba mbingu umeshaikosa tayari.
YEYE: Sawa sawa kwa kuwa Yesu alilaaniwa kwa dhambi zenu.Yeye Yesu atakwenda wapi?
Ndugu zangu tuacheni ushabiki katika dini. Dini si ushabiki someni na waulizeni wachungaji wenu maswali msikubali kufundishwa bila ya kuuliza maswali. Naiusia nafsi yangu na kuwausia ndugu zangu katika ADAM, Yeyote atakayekufa hali ya kuwa ni Mkristo atakwenda motoni. Si maneno yangu bali ya Biblia. 1Wakorintho 15:18. Anayebisha na akafute andiko hilo!
[Sijui ndugu msomaji kama unaendelea kuona nia ya dhati iliyo ndani ya ndugu huyu Mwislamu ya kutaka watu waifahamu ile anayodhani yeye kuwa ndiyo KWELI? Huyu ndugu si kwamba ni mwabudu shetani anayetaka kuwatega Wakristo na watu wengine ili awanase na kuwapeleka kwa shetani; hapaha! Ni mtu ambaye anaamini kabisa kwamba yuko kwenye njia sahihi ya kwenda mbinguni. Unakuja tu kugundua shida kubwa kwenye misingi ya hoja zake. Anatoa maandiko kwa ujasiri kabisa akiamini yanasapoti kile anachokiamini, kumbe wala hayamuungi mkono hata kidogo. Hoja zake zimejengwa kwenye msingi wa UONGO kama nilivyotangulia kusema. Kwa hiyo, hata kama nia yake ni njema, huo msingi wa uongo ndio uangamivu wake – huo ndio utakaomwangamiza. Mara nyingi huwa natoa mfano kwamba, kama una kiu na ukakuta kuna kimiminika fulani kama maji kiko kwenye kikombe nawe ukakinywa, japo nia yako ilikuwa ni njema, yaani kukata kiu, kama kile kimiminika ni sumu, utakufa tu! Nia njema si garantii ya usalama wako; bali ni nia njema pamoja na maarifa sahihi. Yaani, nia njema pamoja na kweli. Basi tukaendelea kujibizana na ndugu huyu.]

MIMI: Rafiki, mbona Waislamu huwa mnatoa reference za ajabuajabu sana. Mwenzako mwingine aliambiwa na ustaadhi wake kuwa Biblia inamwongelea mkuu wa ulimwengu. Akaambiwa kuwa mkuu wa ulimwengu ni Muhammad. Kwa hiyo,  Biblia imemtaja Muhammad. Alipofunuliwa andiko hilo kwenye Biblia na mchungaji mmoja siku moja, akakuta kumbe Biblia inamaanisha ni shetani. Alifedheheka sana. Sasa na wewe unatoa 1 Wakorintho 15:18 kwa ujasiri kabisa. Inasema hivi: Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea. Ulipoona hivyo ukajua, Ehe! Wakristo wamepatikana. Mkasahau kwamba mstari wa 16 unaanza hivi: MAANA KAMA WAFU HAWAFUFULIWI ..... Kwa maana nyingine, kama wafu hawafufuliwi basi ndipo mstari wa 18 unaleta maana hiyo mnayoitamani sana iwe kweli. Njoo kwa Yesu acha ukaidi na ubishi.


Pia, unauliza, kwa kuwa Yesu alilaaniwa kwa dhambi zetu atakwenda wapi? [alilaaniwa na kwa dhambi zako pia]. Mwanao akiiba kisha mahakama ikaamuru alipe faini ya laki moja au aende jela, wewe hutalipa faini hiyo? Je, ukilipa inakuwa sadaka au bado ni faini? Je, unapolipa wewe unageuka kuwa mhalifu? Lakini mwanao huyo akikataa malipo yako mahakama itamwachia? Wewe na mimi ni watenda dhambi na sheria ya Mungu ilishatuhukumu kwenda jehanamu milele. Yesu ni Baba aliyekuja kulipa faini. Wote walioamini juu ya kazi hiyo ya upendo, Mungu anawaacha huru. Wote wanaosema 'sina haja na faini aliyolipa Yesu' wanabakia na hukumu yao na jehanamu inawangoja bila shaka. Kwa hiyo, jibu lako liko wazi sana: Mlipa faini ya mkosaji huwa hageuki kuwa mhalifu!! Njoo kwa Yesu leo.


YEYE: Hayo ni maneno yako si maandiko. Mimi nataka maandiko,"Aliye laaniwa anakwenda wapi? Kwa imani zenu Galatia 3:13 & Kumbukumbu la taurati 21:22 Yesu alifanywa laana kwa dhambi zenu kwa kuwa sijaona andiko la yeye kusamehewa baada ya kuchukua dhambi zenu. Je yeye atakwenda wapi? Na kama kuna andiko la yeye kusamehewa dhambi alizochukua kutoka kwenu naomba unitajie!

[Unamwona tena ndugu huyu. Yaani anajiamini kwelikweli! Unajua, mtu hawezi kujiamini kiasi hiki kama anajua kabisa kwamba amekosea. Lakini kama moyo wake unamwambia kuwa YUKO SAHIHI KABISA, anakuwa na ujasiri mkubwa sana – hata kama hayuko sahihi! Na kama nilivyoanza na mfano mwanzo wa makala haya, maamuzi YOTE ya mtu kama huyu kuhusiana na Yesu na Ukristo, yanakuwa yanatokana na hiki ambacho kimo ndani yake – bila kujali kina ukweli au hakina ukweli. Hakika kabisa, Mungu ni shahidi wangu, hii ndiyo hali ya ndugu zetu Waislamu! Inasikitisha! Basi tukaendelea kuhojiana.]

MIMI: Ndugu, unataka maandiko. Mbona yapo mengi tu.

Rafiki, dhambi haitoki mwilini; inatoka moyoni. Kumbuka hilo. Ndiyo maana dhambi haioshwi kwa maji! Bwana Yesu aliye Mwalimu Mkuu anasema: Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni? BALI VITOKAVYO KINYWANI VYATOKA MOYONI; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi. Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano HAYO NDIYO YAMTIAYO MTU UNAJISI…. (Mt 15:17-20).


Yesu hakuwahi kutenda dhambi. Maandiko matakatifu yanasema wazi: YEYE ASIYEJUA DHAMBI ALIMFANYA KUWA DHAMBI KWA AJILI YETU, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye. (2 Wakor 5:21).


Sasa kwa nini alihesabiwa kuwa mwenye laana? Imeandikwa: Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe KATIKA MFANO WA MWILI ULIO WA DHAMBI, na kwa sababu ya dhambi, ALIIHUKUMU DHAMBI KATIKA MWILI (Warumi 8:3).


Mwili wake ndio uliopata adhabu. Sasa wewe unauliza kwamba, “Sasa yuko wapi?” Na mimi nikuulize, baada ya kufa kinachoendelea huko mbele ya safari huwa ni mwili au huwa ni roho?
 

Naamini unafahamu kuwa kinachoendelea na safari ng’ambo ya mauti ni roho. Na kwa kuwa roho ya Yesu haijawahi kutenda dhambi, unadhani yuko jehanamu au yuko mbinguni? Kama unadhani yuko jehanamu, ataendaje huko wakati hana dhambi?


Maandiko yanasema: roho ile itendayo dhambi itakufa. (Ezekiel 18:4). Sijui kama unaona kuwa katika andiko hili anaongelea roho kufa; si mwili? Kufa kwa roho maana yake kutupwa jehanamu ya milele na Mungu kwa sababu ya dhambi. Sasa, roho ya Yesu haikuwahi kutenda dhambi. Je, bado unadhani iko jehanamu?


Kwa kuhitimisha, Biblia inasema hivi: Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, MWENYE HAKI KWA AJILI YAO WASIO HAKI, ili atulete kwa Mungu; MWILI WAKE AKAUAWA, BALI ROHO YAKE AKAHUISHWA (1 Petro 3:18).


Ndugu, ukimkataa Yesu kama sadaka ya dhambi zako, unabaki na dhambi hizo kwa maana kila roho ya mwanadamu ina dhambi. Kwa hiyo, njia ya kwenda mbinguni imefungwa kwako (kimsingi umejifungia mwenyewe); bali njia ya kwenda kuzimu iko wazi kwako (ambayo umejifungulia mwenyewe)! Uamuzi ni wako. Chagua uzima ulio katika Kristo Yesu ili upone.


………………………………………………


Sijamsikia tena ndugu huyu baada ya kumpa jibu hili. Sijui kama bado anajipanga au ameshaelewa ukweli wa mambo. Lakini ninachotaka kusema ndugu zangu Waislamu, hakuna ubaya kujenga msimamo juu ya maisha yako na yale mambo unayoyaamini. Lakini swali la msingi ni kwamba, “Je, umejenga falsafa ya maisha yako na imani yako juu ya msingi sahihi? Yale uliyoambiwa kuhusiana na Ukristo, Yesu na wokovu wake yametokana na maneno ya kweli? Kupinga Ukristo, hata ukifanya hivyo kwa nguvu zako zote; hadi ukatoa na uhai wako kwa jambo hilo, swali linabaki palepale, je, msingi wako ulikuwa umejengwa kwenye KWELI? Au ulikuwa tu unatumiwa na watu kwa ajili ya maslahi yao wenyewe?


Yapo mafundisho mengi, mengi, mengi mno mnayofundishwa Waislamu kuhusiana na Ukristo ambayo ni UONGO mtupu. Lakini hayohayo ndiyo yamekuwa MSINGI ambao juu yake mmejenga imani yenu na hoja zenu kwa nini hamtaki kuamini kuwa Yesu Kristo ni Mwokozi wa ulimwengu wote; na kwamba bila Yeye, hakuna hata mwanadamu mmoja atakayeingia mbinguni!

Tafakari


Chunguza mambo


Hoji


Chukua hatua

10 comments:

  1. ndugu yangu, biblia huwa inajitafsir yenyewe, tatizo lenu wakristo mnalazimisha ili maana za biblia ziendane na zenu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sana brother Oscar kwa kuitikia makala haya. Mimi ni binadamu siwezi kujisifu kuwa najua kila kitu. Ni kweli kabisa kuna mambo mengi SANA katika Biblia ambayo sijayafahamu; na pia mengi sitayafahamu hadi naondoka kwenye dunia hii.

      Sasa, kuhusiana na makala haya, je, ni kitu gani humu ndani ambacho unadhani kimetafsiriwa kinyume na Biblia inavyojitafsiri?

      Delete
    2. angalia council of nicea ndio msingi wa ukristo ulipoanza ndipo yesu alipewa uungu

      Delete
  2. BARAKA NA AMANI YAKE MUNGU WETU IWE PAMOJA NANYI WOTE MTAKAO SOMA UJUMBE UHU. BIBLIA IPO WAZI SANA KWA WALE WALIO JALIWA NEEMA YAKULIKUBALI NENO LA MUNGU NA NDO WALE WANAO LIELEWA. KUNA WATU WENGI WANAO MZUNGUMZIA YESU KWA NJIA YA MWILI...SASA WEWE KAMA MKRISTO UNAPO MFUNDISHA YESU KWANJIA YA ROHO LAZIMA KUWEPO NA UTATA SABABU WAMEPFUSWA MACHO HAYAHONI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. amen. Baraka na amani ziwe nawe pia ndugu yetu.

      Delete
  3. No need to worry, wewe fanya dhambi zako jc alishazibeba yani kama ni mwezi poa, kama kahaba endelea, kama muongo usiache
    haleluyah

    ReplyDelete
  4. hahaaaa,wakristo imani yenu haieleweki,kuabudu kwenu ni kupiga ngoma na mziki..wapi na wapi hayo?

    ReplyDelete
  5. wapi andiko YESU ALIFUTIWA LAANA ALOIPATA BAADA ya KUTUNDIKWA MSALABANI ndo awe hataingia MOTONI???

    ReplyDelete
  6. yesu hakuwa na dhambi?
    ila alitundikwa msalabni na hivo kulaaniwa?
    maana awekwae kwenye mti amelaaniwa na mungu?

    wapi aya yesu amesafishwa dhambi ili awe msaafi kupokelewa?
    msaada hapo!!!

    alafu biblia inadai kuwa kila mtu atabeba mzigo wake (dhambi)
    ikiwa wewe umezaliwa juzi juzi tu hapa..
    je Furushi gani la kwako alilobeba ikiwa yeye kashabeba ya nyuma?

    ReplyDelete