Sunday, May 18, 2014

Je, Wakristo Waliokufa Wakimwamini Yesu kama Mungu Wamepotea?
Kama kawaida ndugu zangu wa Kiislamu niwapendao sana wanazidi kuzama kwenye dimbwi la udanganyifu. Wananukuu kitabu cha Wakorintho na kusema KWA UJASIRI MKUBWA kwamba tumepotea kwa kumwamini Kristo.

Mungu Muumba wa mbingu na nchi anasema wazi kwenye Biblia kuwa:

“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.” (Hosea 4:6).


Andiko hili halisemi WANAANGAMIA kama ambavyo watu wengi hulitamka; bali linasema WANAANGAMIZWA.Maana yake ni kuwa, kuna kundi la wanadamu linalosambaza udanganyifu; halafu kuna kundi kubwa zaidi la wanadamu linalomeza udanganyifu huo na kudhani kuwa wako salama. Kundi hili la pili, linajumuisha ndugu zangu hawa Waislamu ambao wamemezeshwa maadiko ya Biblia kwa namna ambayo wanadhani wanaelewa kumbe sivyo. Na kinachosikitisha ni jinsi ambavyo huongea kwa UJASIRI MKUBWA kuhusiana na maandiko hayo.


Lakini wasisahau kuwa kutokujua si njia ya kupona hukumu ya Mungu – Bwana anaendelea kusema kwenye andiko hilo hapo juu:  


“kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.”


Maana yake ni kuwa NI WAJIBU WA MTU MMOJAMMOJA KUTAFUTA USAHIHI WA HABARI ZA MUNGU kuliko kumeza chochote unachoambiwa bila kutafuna kwanza.

Basi andiko jingine ambalo kwalo Waislamu wanaangamizwa ni kwa udanganyifu ni wao kusema: NAO WALIOLALA KATIKA KRISTO WAMEPOTEA.

Huwa wanasema hivi wakimaanisha kuwa: Mtu yeyote anayekufa akiwa anamwamini Yesu Kristo [kuwa ni Mungu] basi anakuwa ameingia jehanamu.

Sasa, ukweli uko wapi? Na andiko hilo linapatikana wapi? ---- Liko kwenye kitabu cha Wakorintho wa kwanza:

Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea. Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote. (1Kor 15:18-19).


Kwa hiyo, upotovu na uangamivu wao unatokana na nini? Unatokana hasa na kumezeshwa mambo na kundi fulani la wajanja, huku wao wenyewe hawako tayari kutafuta ukweli wa kile wanachoambiwa. Hebu tuangalie MUKTADHA uliozaa andiko hili, kisha tutajua kama sisi tunaomwamini Kristo tumepotea au la.


Ni muhimu tusome kuanzia nyuma zaidi kuliko kurukia tu kipande cha mstari ambao hata hatujua umeanzia wapi hadi ukafika hapo ulipo. Nitaanzia mstari wa 12, huku nikielezea kila kifungu peke yake. Hatimaye mwishowe ukweli utadhihiri.(1Kor 15:12)  Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu?

Maana yake ni kuwa:

Kwa nini wengine wanasema hakuna kiyama ya wafu wakati Kristo anahubiriwa kuwa amefufuka.


(1Kor 15:13)  Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka;

Maana yake:

Na kama kweli hakuna kiyama ya wafu basi Kristo naye hakufufuka. Lakini kama kuna kiyama ya wafu, basi Kristo naye alifufuka.


(1Kor 15:14-17)  tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure. Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi. Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka. Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu.


Maana yake:

Kama Kristo atakuwa hakufufuka basi sisi tunaohubiri tumefanya kazi bure kuhubiri, tumepoteza muda kuamini, na tumekuwa wahubiri wa jambo la uongo; Na nyie mlioamini mahubiri yetu mtakuwa bado mmo dhambini. [KAMA KRISTO HAKUFUFUKA](1Kor 15:18-19)  Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea. Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote.


Maana yake:

[KAMA KRISTO HAKUFUFUKA] basi wale ambao wamekufa wakiwa wamemwamini Kristo kutokana na hayo mahubiri yetu, watakuwa wamepotea na hata sisi tulio hai na tunaendelea kuyaamini hayo, tutakuwa ni maskini kuliko waislamu, wabudha, na watu wengine wote duniani wasiamini kuwa Yesu alikufa.


(1Kor 15:20)  Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala.

Maana yake:

[KWA KUWA SASA KRISTO AMEFUFUKA] basi, imani yetu si bure, kuhubiri kwetu si bure, waliokufa katika Kristo hawakufa bure, na wala sisi si maskini kuliko watu wote duniani.


Swali kwa Waislamu: Je, andiko hili, yaani andiko lenyewe kama lilivyo,  linamaanisha kuwa wanaokufa wakimwamini Kristo wamepotea au linamaanisha kuwa hawajapotea?


WENYE MACHO WANAONAUTADANGANYWA HADI LINI?MNAANGAMIZWA NA UONGO!!


AMKA!!!!

3 comments:

 1. mungu akubariki mkuu. napenda kujua kwanin ndgu zetu waislamu wanapenda kumtetea mungu wao kwa kupindisha maandiko? kingine ningependa kupata lile fungu yesu aliposema kua torati na manabii vyote vilikua vikimzungumzia yeye. ubarikiwe sana.#kireri

  ReplyDelete
  Replies
  1. Shalom ndugu yangu Kireri.

   Kuhusu kwa nini waislamu wako hivyo walivyo, na pia si wao peke yao, bali na wengine wote wasioikubali Injili ya Kristo iokoayo, Biblia inatuambia kuwa:


   (2Kor 4:3-4) Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.


   Andiko ulilouliza ni hili hapa: (Yoh 5:39) Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia.


   Bwana akubariki.

   Delete
 2. Hapa nimepaelewa sana, Bwana aendelee kuwalinda, ili mzidi kutuelimisha ss tusio elewa.

  ReplyDelete