Kama
kawaida ndugu zangu wa Kiislamu niwapendao sana wanazidi kuzama kwenye dimbwi
la udanganyifu. Wananukuu kitabu cha Wakorintho na kusema KWA UJASIRI MKUBWA kwamba tumepotea kwa kumwamini Kristo.
Mungu
Muumba wa mbingu na nchi anasema wazi kwenye Biblia kuwa:
“Watu
wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.” (Hosea 4:6).
Andiko
hili halisemi WANAANGAMIA kama ambavyo watu wengi hulitamka; bali linasema
WANAANGAMIZWA.
Maana
yake ni kuwa, kuna kundi la wanadamu linalosambaza udanganyifu; halafu kuna
kundi kubwa zaidi la wanadamu linalomeza udanganyifu huo na kudhani kuwa wako
salama. Kundi hili la pili, linajumuisha ndugu zangu hawa Waislamu ambao
wamemezeshwa maadiko ya Biblia kwa namna ambayo wanadhani wanaelewa kumbe
sivyo. Na kinachosikitisha ni jinsi ambavyo huongea kwa UJASIRI MKUBWA kuhusiana
na maandiko hayo.
Lakini
wasisahau kuwa kutokujua si njia ya kupona hukumu ya Mungu – Bwana anaendelea
kusema kwenye andiko hilo hapo juu:
“kwa
kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu
mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto
wako.”
Maana yake
ni kuwa NI WAJIBU WA MTU MMOJAMMOJA KUTAFUTA USAHIHI WA HABARI ZA MUNGU kuliko
kumeza chochote unachoambiwa bila kutafuna kwanza.
Basi
andiko jingine ambalo kwalo Waislamu wanaangamizwa ni kwa udanganyifu ni wao
kusema: NAO WALIOLALA KATIKA KRISTO WAMEPOTEA.
Huwa
wanasema hivi wakimaanisha kuwa: Mtu yeyote anayekufa akiwa anamwamini Yesu
Kristo [kuwa ni Mungu] basi anakuwa ameingia jehanamu.
Sasa,
ukweli uko wapi? Na andiko hilo linapatikana wapi? ---- Liko kwenye kitabu cha
Wakorintho wa kwanza:
Na
hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea. Kama katika maisha haya tu
tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote. (1Kor 15:18-19).
Kwa hiyo,
upotovu na uangamivu wao unatokana na nini? Unatokana hasa na kumezeshwa mambo
na kundi fulani la wajanja, huku wao wenyewe hawako tayari kutafuta ukweli wa
kile wanachoambiwa. Hebu tuangalie MUKTADHA uliozaa andiko hili, kisha tutajua
kama sisi tunaomwamini Kristo tumepotea au la.
Ni muhimu
tusome kuanzia nyuma zaidi kuliko kurukia tu kipande cha mstari ambao hata
hatujua umeanzia wapi hadi ukafika hapo ulipo. Nitaanzia mstari wa 12, huku
nikielezea kila kifungu peke yake. Hatimaye mwishowe ukweli utadhihiri.
(1Kor
15:12) Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya
kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya
wafu?
Maana
yake ni kuwa:
Kwa
nini wengine wanasema hakuna kiyama ya wafu wakati Kristo anahubiriwa kuwa
amefufuka.
(1Kor
15:13) Lakini kama hakuna kiyama ya
wafu, Kristo naye hakufufuka;
Maana
yake:
Na
kama kweli hakuna kiyama ya wafu basi Kristo naye hakufufuka. Lakini kama kuna
kiyama ya wafu, basi Kristo naye alifufuka.
(1Kor
15:14-17) tena kama Kristo hakufufuka,
basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure. Naam, na sisi tumeonekana
kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa
alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi. Maana kama wafu
hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka. Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni
bure; mngalimo katika dhambi zenu.
Maana
yake:
Kama
Kristo atakuwa hakufufuka basi sisi tunaohubiri tumefanya kazi bure kuhubiri,
tumepoteza muda kuamini, na tumekuwa wahubiri wa jambo la uongo; Na nyie mlioamini
mahubiri yetu mtakuwa bado mmo dhambini. [KAMA KRISTO HAKUFUFUKA]
(1Kor
15:18-19) Na
hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea. Kama katika maisha haya tu
tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote.
Maana
yake:
[KAMA
KRISTO HAKUFUFUKA] basi wale ambao wamekufa wakiwa wamemwamini Kristo kutokana
na hayo mahubiri yetu, watakuwa wamepotea na hata sisi tulio hai na tunaendelea
kuyaamini hayo, tutakuwa ni maskini kuliko waislamu, wabudha, na watu wengine
wote duniani wasiamini kuwa Yesu alikufa.
(1Kor
15:20) Lakini sasa Kristo amefufuka
katika wafu, limbuko lao waliolala.
Maana yake:
[KWA KUWA SASA KRISTO AMEFUFUKA] basi, imani
yetu si bure, kuhubiri kwetu si bure, waliokufa katika Kristo hawakufa bure, na
wala sisi si maskini kuliko watu wote duniani.
Swali kwa Waislamu: Je, andiko hili, yaani
andiko lenyewe kama lilivyo, linamaanisha kuwa wanaokufa wakimwamini Kristo
wamepotea au linamaanisha kuwa hawajapotea?
WENYE MACHO WANAONA
UTADANGANYWA HADI LINI?
MNAANGAMIZWA NA UONGO!!
AMKA!!!!
mungu akubariki mkuu. napenda kujua kwanin ndgu zetu waislamu wanapenda kumtetea mungu wao kwa kupindisha maandiko? kingine ningependa kupata lile fungu yesu aliposema kua torati na manabii vyote vilikua vikimzungumzia yeye. ubarikiwe sana.#kireri
ReplyDeleteShalom ndugu yangu Kireri.
DeleteKuhusu kwa nini waislamu wako hivyo walivyo, na pia si wao peke yao, bali na wengine wote wasioikubali Injili ya Kristo iokoayo, Biblia inatuambia kuwa:
(2Kor 4:3-4) Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
Andiko ulilouliza ni hili hapa: (Yoh 5:39) Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia.
Bwana akubariki.
Hapa nimepaelewa sana, Bwana aendelee kuwalinda, ili mzidi kutuelimisha ss tusio elewa.
ReplyDelete