Friday, October 13, 2017

Kwa nini tunasema ISIS ni Waislamu swafi?


Ndugu zetu husema kwa msisitizo kabisa kwamba Muhammad ndio kipimo chao cha ucha Mungu wao.
Kwa hiyo, kila mwislamu angependa kufikia ngazi ya mtume wao, Muhammad kwa:
-       kusema aliyosema
-       kufanya aliyofanya
-       kuwaza aliyowaza
maana hayo si ndiyo mema?
 Katika mji wa Madina kulikuwa na kabila la Wayahudi walioitwa Banu Qurayza. Hawa walivamiwa na Muhammad na kundi lake katika mapigano yaliyodumu kwa siku zipatazo 25. Walizidiwa nguvu na ku-surrender.
Muhammad alimchagua sahaba wake mmoja aliyeitwa Sa'd ibn Mu'adh ili awe ndio mwamuzi wa nini kifuate baada ya Banu Qurayza kusalimu amri.
Sa'd ibn Mu'adh aliamua kuwa wanaume wote wa Banu Qurayza wauawe, mali zao zitwaliwe na wanawake na watoto wao wachukuliwe mateka.
Muhammad akakubali.
Sasa nini kilitokea kwa wale waliohukumiwa mauti?

Tunasoma kwenye Al- Tabari 8:35 and ibn Ishaq:464

"The Jews were made to come down, and Allah's Messenger imprisoned them. Then the Prophet went out into the marketplace of Medina, and he HAD TRENCHES DUG in it. He sent for the Jewish men and had them beheaded in those trenches. They were brought out to him in batches. They numbered 800 to 900 boys and men."
…………..
Maana yake:
Wayahudi waliletwa na Mjumbe wa Allah akawaweka kifungoni. Kisha Mtume akaenda kwenye soko la Medina, na akaamuru ichimbwe mitaro ndani yake. Akaagiza wale wanaume wa Kiyahudi waanze kuletwa na akaamuru wakatwe vichwa (wachinjwe) kwenye ile mitaro. Waliletwa kwake kwa makundi makundi. Jumla yao ilifikia wanaume na wavulana 800 hadi 900.

……………
Huyo ndio Muhammad ambaye ni kipenzi cha Allah na MFANO SAHIHI wa kufuatwa na Mwislamu yeyote.

Maswali yetu sisi wengine ni kuwa:
1.     Wewe ni nani unayesema kuwa Boko Haram si waislamu safi kutokana na kitendo chao cha kuteka wasichana 200 wa shule wakati Muhammad aliteka kabila zima?
2.     Wewe ni nani kusema ISIS sio waislamu safi wakati nao huchimba mitaro na kuua watu ndani yake kama Muhammad alivyofanya? Au kwa sababu wao wanatumia bunduki badala ya mapanga?

Ndugu zangu Waislamu, najua mtadai kuwa Banu Qurayza walivunja mkataba ndio maana walistahili kutendewa hivyo.

Hicho nacho ni kichekesho kikubwa kwa sababu ifuatayo.

Ukikutana na profesa hataki kufundisha na sababu anayotoa ni kuwa, “Mbona wanafunzi wenyewe hawanifundishi?” – hivi kama uko karibu hautamzabua kwenzi kweli?

Ninyi si mnaamini kuwa ndio mlio na neno la Mungu?
Ninyi si mnaamini kuwa wasio waislamu wako upotevuni kwa sababu hawajui njia za Mungu?
Sasa aliye nje ya Mungu akikosa, wewe si ndio profesa wa kumfundisha?
Sasa kama na wewe unafanya afanyayo huyo unayemwita kafiri, wewe una nini cha zaidi?
Yaani unataka eti yeye aliye mpagani ndio atende tendo jema kwanza, NDIPO na wewe umtendee tendo jema! Kha!

Bado sisi tunadhani, kama kweli Muhammad ndio mfano bora wa Uislamu, basi ISIS na Boko Haram ni waislamu wazuri sana.

…………….
Yesu ni njia pekee ya uzima.
Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima. (Yohana 8:12)
Tafakari.
Chukua hatua.

No comments:

Post a Comment