Friday, October 13, 2017

Lugha iliyo safi SIO Kiarabu



Ndugu zetu Waislamu wanasikitisha sana; tena sana!

Katika Sefania 3:9 imeandikwa:
Maana hapo ndipo nitakapowarudishia mataifa LUGHA ILIYO SAFI, wapate kuliitia jina la Bwana, wamtumikie kwa nia moja.

Ndugu zetu wanadai huo ni utabiri wa lugha ya Kiarabu ambayo ndiyo inayotumiwa kwenye Uislamu. Duh!


Wakati nabii Sefania akiandika ujumbe huu, Mungu (Yahweh) alikuwa ameghadhibikia sana mataifa mbalimbali kwa sababu ya kupenda uovu badala ya kupenda haki inayotokana na kumtii Yeye.

Ndipo akasema:
Basi ningojeni, asema Bwana, hata siku ile nitakapoondoka kuteka mateka; maana nimeazimia kuwakusanya mataifa, ili nizikutanishe falme, nipate kuwamwagia ghadhabu yangu; naam, ukali wote wa hasira yangu; kwa maana dunia yote itateketezwa kwa moto wa wivu wangu. Maana HAPO NDIPO NITAKAPOWARUDISHIA MATAIFA LUGHA ILIYO SAFI, wapate kuliitia jina la Bwana, wamtumikie kwa nia moja. (Sefania 3:8-9)

Hebu tujiulize tu swali rahisi la kimantiki:
Kwa kuwa hapa Mungu ana hasira kali dhidi ya TATIZO LA UOVU; 
na kwa kuwa SULUHISHO lake ni kuleta LUGHA SAFI itakayosababisha mataifa yote yamwabudu kwa nia moja iliyo safi; 
na kwa kuwa ninyi ndugu Waislamu mnadai lugha hiyo ni Kiarabu – 
je, iwapo wewe ndugu mwislamu una vijana au binti zako ambao wamezama kwenye dhambi, mfano uzinzi, uuaji, dawa za kulevya, ujambazi, nk – 
JE, UKIWAFUNZA KIARABU WATAPONA? 
Je, LUGHA INAWEZA KUBADILI MIOYO?
Je, lugha inaweza kumfanya jambazi akawa mtu mwema?  
Je, jela zinaweza kukosa watu kwa iwapo utawafunza wafungwa wote Kiarabu kweli?

Mbona mnaangamizana wenyewe ndugu zetu kwa kulishana uongo?

Yesu ni Jibu la maisha.
Tafakari
Chukua hatua

No comments:

Post a Comment