Zamani wakati wa
Agano la Kale, ziliwahi kutokea falme na mamlaka kubwa zilizotawala dunia nzima
ya wakati ule.
Kwa mfano, dola ya
mkono wa chuma ya Rumi ilitawala dunia kwa mabavu kwa miaka 1500. Lakini iko
wapi leo?
Zimepita tawala
nyingi hapa duniani na zingine bado zinaendelea kuja. Na kila utawala UNAJARIBU
kuongoza dunia kwa madai kuwa wenyewe ndio unaofaa.
Hata hivyo ni wazi
kuwa karibu kila utawala umesababisha mateso tu. Serikali zimeleta mateso kwa
watu. Dini zimeleta mateso kwa watu. Siasa, teknolojia, na hata mifumo mifumo
mbalimbali kama vile ujamaa, ukomunisti, ubepari, nk – vyote hivyo vimejaribu
na kushindwa kuwa syuluhu – badala yake vimekuwa vyanzo vya tabu na mateso ya
aina mbalimbali kwa mwanadamu.
Lakini zamani kabla
ya Yesu, alitokea mfalme kwenye nchi ya Babeli (Iraki) aliyeitwa Nebukadreza.
Aliota ndoto ambayo nabii Danieli anaitaja:
Danieli 2:31-33
Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama,
sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi
sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha. Na sanamu hii
kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya
fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba; miguu
yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo.
Sanamu hii iliwakilisha tawala
mbalimbali za dunia hii. Hizi ni kama mawe yaliyochongwa na wanadamu.
Ndipo Danieli akapewa
tumaini la uhakika. Mungu wa mbinguni alimpa ujumbe huu ambao ulikuwa ni kile
kitakachotokea baada ya hekaheka za wanadamu.
Danieli 2:34-35
Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa
bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya
chuma na udongo, likaivunja vipande vipande. Ndipo kile chuma, na ule udongo,
na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja
vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo
ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo
sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.
Lilitokea jiwe
jingine ambalo halikuchongwa na mwanadamu. Lilisambaratisha falme na tawala na
dini na jitihada ZOTE za wanadamu ili kwamba kile kilichotoka kwa Mungu
kitawale dunia YOTE milele.
Jiwe hilo ni Yesu
Kristo na Ufalme wake.
Mathayo 4:17
Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri,
na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
Uislamu una miaka 1400 sasa. Hata kama
utaishi tena miaka 5000 mingine, hiyo ni kama dakika tu mbele ya kipindi
kinachoitwa MILELE.
Ubepari utasagwasagwa na kutoshwa na
Jiwe la mbinguni.
Umoja wa mataifa utasagwasagwa na
kutoshwa na Jiwe la mbinguni.
Umoja wa Ulaya utasagwasagwa na
kutoshwa na Jiwe la mbinguni.
UISLAMU UTASAGWASAGWA NA KUTOSHWA NA
JIWE LA MBINGUNI.
It’s just a matter of time.
No comments:
Post a Comment