Sunday, March 24, 2013

Juhudi za Kupinga Ukristo za Mwanaharakati wa Kundi la Ahmadiah Kutoka Pakistani Zamfanya Aachane na Uislamu



Nusrat Aman alikuwa ni mwanaharakati wa kiislamu wa kundi la Ahmadiah kule Pakistani. Siku moja aliamua kuingia kanisani ili akamwulize mchungaji ni kwa nini hasa hataki kuwa mwislamu ilhali unabii wote umeshatimizwa ndani ya Muhammad? Nusrat aliishia kupata aibu, hasira na hatimaye wokovu …!


Je, ilikuwaje? Endelea kusoma ushuhuda wake wenye kichwa kisemacho "Kwa nini niliamua kuwa Mkristo?" ambao unafungua macho na mioyo kwa kuwa ni watu wengi walio katika kundi alimokuwa Nasrat hapo zamani.

Injili ya Barnaba - Beleshi Linalochota Waislamu na Kuwatupia Kwenye Shimo la Kuzimu



Ulimwengu wa Kiislamu, kama kawaida yake, unatia juhudi kubwa sana katika kuuchafua Ukristo ili angalau uweze kuendelea kuwashikilia walio ndani yake; na pale inapowezekana, kuwadanganya Wakristo wasiojua Ukristo wala Uislamu.

Kuna mambo mawili makubwa ambayo huwa yananishangaza sana kuhusiana na masuala ya kiroho. Kwanza ni jinsi ambavyo wakuu wa dini wa Kanisa Katoliki wanavyotumia miaka na miaka kusomea dini na Biblia, kisha wanakuja kuishia kufundisha mambo yaliyo nje ya Biblia!!! Kwa mfano, wanawaambia waumini wao kuwa wafu wanatuombea kule mbinguni au kwamba unaweza kufanya misa huku duniani halafu ndugu yako aliyekufa akiwa na dhambi na, kwa ridhaa yake alikataa wokovu, eti atasamehewa dhambi na Mungu atamuingiza mbinguni!!!

Thursday, March 21, 2013

Aliyekuwa Ustaadhi na Hakimu wa Mahakama ya Sharia Akutana na Injili ya Yesu Kristo na Kuokoka – Sehemu ya 2



Ahmed alikuwa ni injinia. Baadaye alishawishiwa na Ulama mmoja na kupandikiziwa chuki dhidi ya Wakristo na Wayahudi kiasi kwamba aliamua kuacha kazi yake na kwenda kusomea masomo ya dini ya Kiislamu (licha ya mama yake kupinga sana).

Masomo hayo yalimwezesha kuwa hakimu wa mahakama ya sharia. Kutokana na ukandamizaji mkubwa aliouona kwenye mahakama hizo na kukosekana kwa haki na pia kukosekana kwa msimamo juu ya tafsiri sahihi ya sheria za kiislamu, moyo wake ulikosa kabisa amani.

Kwa neema za Yesu Kristo, Ahmed alifunguliwa macho yake na sasa anajiuliza ilikuwaje akaamini Uislamu?

Ufuatao ni ushuhuda wake kwa maneno yake mwenyewe ambao ameupa kichwa cha habari: “Njia ya Allah Kuelekea Jehanamu au Njia ya Yesu Kuelekea Mbinguni.”

Kwa kuwa hii ni sehemu ya 2, ili kupata picha kamili, tafadhali anza na Sehemu ya 1 HAPA.

Sunday, March 17, 2013

Maswali Yanayonitatiza Kuhusiana na Quran



Ibra na Waislamu wengine, kumekuwa na kawaida kwa ulimwengu wa Kiislamu kufanya kila juhudi kuonyesha kwamba Biblia imepotoshwa, ingawaje jambo hilo si kweli hata kidogo. Ukiachilia mbali makosa ya kibinadamu ya hapa na pale ambayo yanaingia kutokana na ukweli kwamba Biblia imetafsiriwa na inaendelea kutafsiriwa mara nyingi sana, hakuna makosa ya makusudi yanayofanywa ili kupotosha au kuficha ukweli.

Na juhudi hizi zote zinafanywa ili kutaka kuonyesha kwamba  Quran ni neno la Mungu la kweli ambalo halijapotoshwa hata kidogo. Basi mimi naomba mnisaidie majibu ya maswali haya machache kati ya mengi:

Majibu Yangu kwa Ibrabura - Sehemu ya 2



JE, BIBLIA NI KITABU KILICHOPOTOSHWA?

Yeremia 8:8 inasema kwamba: Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.


Waislamu walipoona maneno haya: “Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo,” kama kawaida, wakajua kuwa huu tayari ni ushahidi kwamba Biblia imetiwa maneno ya uongo, kwa hiyo si Neno la Mungu na haiwezi kuaminika.


Lakini mara zote ni lazima kwenda kwenye muktadha wa kila andiko au hoja ili kuona kama kweli hoja hizo zina nguvu ya kusimama.

Biblia na Quran ni Vitabu Vyenye Nguvu Sana



Historia ni kama ghala kubwa ambamo kumehifadhiwa kila kitu. Tunapochungulia kwenye ghala hili, tunaweza kujifunza kuhusiana na wapi tumetokea, na hatimaye wapi tuliko na kule tunakoelekea.

Bila shaka Biblia na Quran ni vitabu viwili ambavyo vina umuhimu mkubwa sana kwa wanadamu na ulimwengu. Hivi ni vitabu ambavyo ndivyo vinavyoumba maisha halisi ya idadi kubwa sana ya watu. Haya si tu maisha ya kula, kunywa na kuvaa hapa duniani, lakini pia vinaaminika kuwa vimebeba hatima ya milele yote kuhisiana na kila mwanadamu.

Friday, March 15, 2013

Majibu Yangu kwa Ibrabura - Sehemu ya 1




Katika makala haya, ninajibu hoja zako rafiki yangu Ibra, ambazo umezitoa kwenye sehemu ya ‘comments’ kwenye makala yangu mengine yenye jina:  Je, Yesu aliagiza wafuasi wake wawaue maadui wa Yesu? Unaweza kusoma HAPA.


Ninatoa majibu yangu kama makala tofauti kwa sababu kuu mbili. Kwanza ni kuwapa fursa watu wengine waweze kujifunza kutokana na mjadala wetu na hata kuchangia au kutusahihisha pale tunapokosea. Pili, kutokana na urefu wa majibu yangu, ni rahisi kuyatoa kama makala kuliko maoni (comments), maana maoni ya mara moja hayatakiwi kuzidi herufi takribani 4,000 hivi.

Tuesday, March 5, 2013

Mpiganaji wa Hezbollah Akutana na Yesu na Kuokoka – Sehemu ya II





Afshin Javid alikuwa ni askari wa Hezbollah ambaye aliyatoa maisha yake kikamilifu kwa ajili ya Allah. Katika maisha yake yote, alijifunza kumtii Allah na alikuwa tayari kufanya lolote, ikiwa ni pamoja na kufa kwa ajili ya Allah.


Lakini baada ya kukutana uso kwa uso na Bwana Yesu, kila kitu kilibadilika. Sikiliza ushuhuda wake huu wenye nguvu sana, ambao si  tu kwamba utakutoa machozi, kama yeye mwenyewe anavyoeleza kwa machozi mengi, bali pia utajua jinsi Bwana Yesu alivyo Mungu Mkuu na wa kweli ambaye, kila anayemtafuta kwa moyo wa kweli, anamwona.


Hii ni sehemu ya pili ya ushuhuda wake. Ili kupata picha kamili, tafadhali anza kwa kusikiliza au kusoma ushuhuda wake, sehemu ya kwanza HAPA.

Monday, March 4, 2013

Je, Yesu Aliagiza Wafuasi Wake Wawaue Maadui wa Yesu?


Katika makala yangu niliyoipa kichwa kisemacho: Je, Muhammad Ametabiriwa Kwenye Biblia? – Sehemu ya II, yaliyo hapa; ambayo kimsingi ninaonyesha kimaandiko kwamba Muhammad kamwe hajatabiriwa kwenye Biblia, rafiki yangu Ibra kwenye sehemu ya maoni (comments) umenipa changamoto mojawapo ya muhimu sana.

Unasema: Mr. James, Kitu kibaya kwako ulichokiona kimeandikwa ndani ya qurani ni juu kuwachinja watu waovu? Sasa kama ndio hivyo, wewe hujasoma biblia au biblia hauijui vizuri. Unafanana na mtu wa kucopy na kupaste.

Friday, March 1, 2013

Majibu Yangu Kwa Ibra Kuhusu Wana wa Ibrahimu - Isaka na Ishmaeli



 Ishmaeli na mama yake (Hajiri) 
wanafukuzwa nyumbani kwa Ibrahimu

Katika makala yangu yenye kichwa kisemacho: Je, Muhammad Ametabiriwa Kwenye Biblia? – Sehemu ya II, ndugu yangu Ibra amenipa changamoto kadha wa kadha ambazo naziheshimu na nimezitafakari vizuri. Unaweza kuzisoma kwa ukamilifu wake kwenye sehemu ya ‘comments’ mwisho kabisa wa makala yaliyo hapa.


Mjadala wangu na Ibra unatokana na hoja yake kwamba Muhammad alitumwa kwa watu wote lakini, Ibra anasema, Yesu alitumwa kwa ajili ya wana wa Israeli tu, kitu ambacho mimi nimemweleza kuwa si kweli kwamba Yesu alitumwa kwa Israeli tu. Hoja zake na majibu yangu viko kwenye sehemu ya hiyohiyo ya maoni (comments) mwishoni mwa makala yaliyo hapa.