Friday, November 15, 2013

Urithi wa Uislamu kutoka kwenye dini za kipagani za Uarabuni – Sehemu ya 2




Ka’aba

Katika sehemu ya 1 ya makala haya tuliangalia kuhusu asili ya Allah. Katika sehemu hii ya 2 tutaongelea kuhusiana na mji wa Makka na ka'aba, ambayo ni madhabahu kuu ya Uislamu.

Mji wa Makka ndio kitovu cha Uislamu duniani. Kwenye mji huu ndiko iliko Ka’aba, au kama wanavyoamini na kuiita Waislamu Bait – ul- Haram; au Bait – ul- Allah, yaani ‘nyumba ya Allah’ au ‘nyumba ya Mungu’. Na kila Mwislamu kokote duniani anatakiwa kuswali swala 5 kila siku huku akielekeza uso wake Makka iliko hiyo nyumba ya Mungu wao. Vilevile, kila mmoja wao anatakiwa kwenda Makka kuhiji walau mara moja katika maisha yake, maana hija ni moja ya nguzo kuu katika Uislamu. Kwa maana nyingine, Ka’aba ndiyo madhabahu kuu katika Uislamu.

Monday, November 11, 2013

Urithi wa Uislamu kutoka kwenye dini za kipagani za Uarabuni - sehemu ya 1





Allah alitokea wapi?

Uislamu unajinadi kwamba Allah ndiye Mungu yuleyule aliyejishughulisha ya Wayahudi tokea nyakati za Ibrahimu katika Agano la Kale. Je, jambo hilo ni kweli?

Uislamu ulianza na Muhammad kwenye miaka 600 baada Kristo. Je, kabla yake imani za Waarabu zilikuwaje? Je, yako mambo yoyote kutoka kwenye imani hizo ambayo yaliingia kwenye Uislamu? Kwa maneno mengine, je, Uislamu hauna upagani ndani yake?

Fuatana nami kwenye makala haya marefu yanayochambua chimbuko la Uislamu ili tuweze kuona iwapo upo uhusiano wowote kati ya Uislamu na upagani uliokuwa ukitawala miongoni mwa jamii za Waarabu kabla ya kutokea kwa Muhammad?

Sunday, August 25, 2013

Mungu Amwonyesha Nabeel Njia ya Kweli Kati ya Uislamu na Ukristo - Sehemu ya 2





Katika sehemu ya kwanza ya ushuhuda huu wa Nabeel, aliyekuwa Mwislamu kisha akakutana na Bwana Yesu na kupokea wokovu, tuliona jinsi ambavyo alimwomba Mungu ampe maono yatakayomwonyesha imani ya kweli. Alionyeshwa misalaba kwenye maono lakini yeye akasema labda ni macho yake tu yamemchezea mchezo. Kwa hiyo, alimwomba tena Mungu kwamba, kama yale maono yalitoka kwake, basi ayathibitishe kwa ndoto. Je, Mungu alifanya nini? Tafadhali endelea kusoma sehemu hii ya pili.

Saturday, August 24, 2013

Mungu Amwonyesha Nabeel Njia ya Kweli Kati ya Uislamu na Ukristo - Sehemu ya 1





Nabeel alizaliwa na kukulia kwenye familia na maisha ya kiislamu. Uislamu ulikuwa ni kila kitu kwake. Lakini wakati ulipofika wa yeye kujua jema na baya, alianza kujihoji kuhusu maisha yake, Mungu wake, na hatima yake ya milele. Hatimaye alimwomba Mungu amwonyeshe kweli. Je, nini kilitokea? Tafadhali fuatilia sehemu hii ya kwanza ya ushuhuda huu.

Friday, July 26, 2013

Yesu Aongea na Binti wa Kiislamu; Binti Aokoka





Sharoni hakuwa Mkristo bali alikuwa ni binti wa Kiislamu. Na wala hakuwa amewahi kujifunza habari za Yesu na Ukristo. Lakini Bwana Yesu mwenyewe alimfuata na kujidhihirisha kwake. Je, ilikuwaje, na nini kilitokea baada ya hapo? Tafadhali fuatilia ushuhuda huu wenye nguvu na unaodhihirisha upendo na uweza na uungu wa Bwana Yesu.

Sunday, July 14, 2013

Toufik Alikuwa Mwislamu Lakini Alimwita Yesu, Leo Ameokolewa na Hajawahi Kujuta



Ufuatao ni ushuhuda wa Toufik, ambaye alikuwa ni Mwislamu lakini alikutana na injili ya Bwana Yesu na kubadili welekeo ambao hajaujutia; na hata anapoelezea neema hii ya wokovu wa Yesu aliyoipata, machozi yanamtoka. Pia machozi yanamtoka zaidi anapowafikiria ndugu zake Waislamu ambao wanapambana kwa jitihada nyingi wakijaribu kumpendeza Mungu kwa njia ya matendo yao ya kidini. Toufik analia anapotambua kuwa yote hiyo wanayofanya ni kazi bure kwa kuwa hawajagundua ziri ambayo na yeye, miaka mingi iliyopita, alikuwa hakuijua.

Thursday, July 11, 2013

Kufa kwa Yesu Kristo Maana Yake Nini?




Utakatifu

Mungu ni mtakatifu. Kutenda dhambi ni kukosa utii kwa Mungu. Mungu anasema kwenye Neno lake: Basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu. (Walawi 11:45).

Pia imeandikwa: Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu (1 Petro 1:15).

Kwa kifupi, kuwa mtakatifu maana yake ni kutokuwa na dhambi yoyote. Mungu kamwe hawezi kufumbia macho dhambi hata iwe ni moja. Kamwe! Hafumbii macho hata zile dhambi ambazo sisi tunaziona ni ndogo sana.

Saturday, July 6, 2013

Je, ni Kweli Quran Haijawahi Kubadilika na Wala Haina Mkono wa Mwanadamu Ndani Yake?




Utangulizi
Rafiki yangu Ibra, amekuwa akinishambulia sana kwa kusema kuwa Biblia ni kitabu kisichoaminika bali Quran ndiyo inayopaswa kuaminiwa. Hoja yake kuu, kama ilivyo kwa Waislamu wengine wengi ni kwamba, Biblia imeingizwa maneno ya kibinadamu kiasi kwamba yale ambayo Mungu aliyateremsha ni kama hayapo tena leo.

Katika makala haya ninapenda tuangalie swali kwamba: Je, ni kweli Quran ni kitabu ambacho hakijawahi kubadilika? Je, ujumbe wake ndio uleule ambao aliteremshiwa Muhammad na Allah? Je, ni kitabu cha kuaminika kuliko Biblia kama wanavyosema Waislamu?

Friday, July 5, 2013

Je, Biblia Ina Vitabu Vingapi?




Vitabu 73 au 66?
Leo duniani kuna Biblia yenye vitabu 73 na yenye vitabu 66. Waislamu wamekuwa wakitumia suala hili kama silaha ya kushambulia Biblia kwamba ni kitabu kisichoaminika, wala hakiwezi kumfikisha mtu mbinguni.

Kwa mfano, ndugu yangu Ibra ambaye amekuwa msomaji na mchangiaji mzuri sana wa blog hii ameniuliza kama ifuatavyo:
James, naomba majibu kwa maswali yafuatayo:
-Biblia original kabisa iliyoandikwa na roho mtakatifu ina vitabuvingapi?
-Kitabu cha Danieli kina sura 12 au 14?
-Biblia yenye vitabu 73 na ile ya 66 ipi ya kweli? Je! Hapa kuna mkono wa roho mtakatifu au ubinadamu?
Ukweli unabaki palepale kwamba biblia sio kitabu cha kutegemea sana kwa mambo ya mungu. Hapa duniani biblia ninazojua mimi ziko zaidi ya tano. Na zote zimepishana kwa namba ya vitabu vilivyopo.
Sasa hapo mimi nabaki nashangaa, niamini biblia gani kati ya hizi? Ubabaishaji, kweli haimo.
Tafakari. Jihoji. Kweli imo ndani yako! Soma Qur'ani tukufu.

Wednesday, June 26, 2013

Swali kwa Waislamu Kuhusu Kupotoshwa kwa Biblia




Je, Biblia ni Kitabu Kilichopotoshwa na Wanadamu?



Waislamu wanashikilia SANA kwamba Biblia imepotoshwa; na kwamba Quran ndicho kitabu cha kweli chenye ujumbe wa kweli wa Mungu aliye hai.

Baada ya Yesu kuondoka Duniani, Quran ilikuja miaka zaidi ya 600 baadaye. Biblia ilishakuwapo kwa maelfu ya miaka kabla ya hapo.

Baada ya Quran kuandikwa, ikasema mengi kuhusiana na Biblia, yakiwamo machache yafuatayo:

Sunday, June 9, 2013

Akef Tayem, Mwislamu Kutoka Palestina Akutana na Bwana Yesu na Kuokoka – Sehemu ya 3





Mpendwa msomaji na mpenzi wa blog hii, naamini ulishasoma sehemu ya 1 na ya 2 za ushuhuda huu wa Akef. Hii ni sehemu ya 3 na ya mwisho inayoonyesha ukuu, upendo na uweza wa Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, yaani Yesu Kristo. Karibu usome sehemu hii na Bwana Yesu akubariki.

Sunday, June 2, 2013

Akef Tayem, Mwislamu Kutoka Palestina Akutana na Bwana Yesu na Kuokoka - Sehemu ya 1





Yafuatayo ni mahojiano kati ya mtangazaji, Sid Roth na Akef Tayem. Akef Tayem anatokea Palestina. Alikuwa ni Mwislamu lakini sasa anamwamini Yesu kama Bwana na Mwokozi wake. Pia anawapenda sana Wayahudi ambao zamani aliwachukia kwa moyo wake wote. Je, nini kilitokea? Hakika Bwana Yesu anahusika humo! Karibu ukutane na Bwana wa mabwana anayeweza kubadilisha maisha yako kwa namna ya kushangaza.

Thursday, May 16, 2013

Injili ya Yesu na Muujiza wa Yesu Vyamfanya Nadereh Aachane na Uislamu





Nadereh ni mwanamke aliyekuwa Mwislamu ambaye aliishi kulingana na sheria na taratibu za dini ya Kiislamu. Lakini katika maisha yake ya kumtafuta Mungu, alikutana na vikwazo au upungufu kadhaa. Hatimaye, alijikuta akibadili mwelekeo wake na kupokea wokovu wa Yesu Kristo. Je, ni nini kilitokea? Ni kwa nini hajutii uamuzi wake huo? Ungana naye ili uweze kujifunza jinsi Mungu anavyokupenda na kile alichokuandalia kwa ajili ya maisha haya na yale yajayo.

Monday, May 13, 2013

Kutoka Kwenye Uislamu Hadi Kumkubali Yesu Kristo





Naeem alikuwa ni Mwislamu tangu utoto wake. Ulifika wakati ambapo alikutana na Yesu Kristo. Matokeo yake, aliweza kuyajua makusudi ya kuumbwa kwake. Na sasa anamshangilia Mwokozi na Muumba wake ampendaye, yaani Yesu Kristo. Je, ilikuwaje? Tafadhali soma ushuhuda wake ufuatao:

Friday, May 3, 2013

Mwanamke wa Kiislamu Kutoka Palestina Aliyetokewa na Bwana Yesu na Sasa Ameokoka





Khalida ni mwanamke aliyekuwa Mwislamu, lakini baada ya kukutana na Bwana Yesu na kutembelea mbinguni, kila kitu kilibadilika kwake. Je, ni kitu gani kilitokea maishani mwake hadi kufikia kupelekwa mbinguni na Bwana Yesu? Tafadhali soma au sikiliza ushuhuda huu wa kweli wenye nguvu ambao utakuonyesha upendo, uweza, mamlaka na nguvu za Bwana Yesu, ambavyo vyote viko kwa ajili yako pia. Khalida anafanyiwa mahojiano na Sid Roth.

Sunday, April 21, 2013

Mamilioni ya Waislamu Afrika Wanamkimbilia Yesu Kristo Isivyo Kawaida





 “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika 
ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa 
yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja” 
(Mathayo 24:14).

Ukisoma kurasa mbalimbali za kwenye mtandao juu ya kukua kwa dini ya Kiislamu, utakuta wengi wanasema kwamba Uislamu ni dini inayokua kwa kasi sana. Je, hilo ni kweli? Ni jambo gani linaloonyesha ukweli wa hoja hiyo?

Lakini tunao ushahidi wa Neno la Kristo kwamba siku za mwisho (yaani hizi tulizo nao), Injili itahubiriwa ulimwenguni kote. Pia, Mungu Yehova anaahidi kuwa hizi ni siku za kumwaga Roho wake kwa wanadamu wote. Hakika hizi ni nyakati za Injili ya Yesu Kristo kusonga mbele na kushinda na kubomoa kila upinzani na ukuta uliojengwa na adui ili kuwazuia wanadamu kumjua Mungu wa kweli na Mwokozi pekee, Yesu Kristo.

Je, Mtume Muhammad Yuko Wapi Hivi Leo?






Mungu hutufunulia mambo mbalimbali kupitia watumishi wake mbalimbali ili kutujulisha yale yaliyopo na hata yajayo; katika ulimwengu huu na pia ule ujao. Wapo watu wengi ambao Mungu amewatumia kutufahamisha juu ya mbingu na hata juu ya kuzimu.

Bo Ra Choi ni mchungaji kutoka Korea ya Kusini. Mchungaji huyu amekuwa akionyeshwa maono mbalimbali na Mungu kuhusu mambo ya ulimwengu wa roho. Mojawapo ya maono aliyoonyeshwa yanamhusu Muhammad, mtume wa Uislamu.

Je, Muhammad yuko wapi hivi leo? Katika video hii, mchungaji Bo Ra Choi anafikisha kwetu ujumbe kwa namna ambavyo alisikizishwa Muhammad akisema kule aliko sasa.

Kwa maana nyingine, ananukuu moja kwa moja maneno ya Muhammad ili kwamba iwe ni kama vile tunamsikia Muhammad akizungumza.

Tafadhali zikiliza kwa makini video hii, kisha utaupata ujumbe wa Mungu anaouleta kwetu kupitia mtumishi wake, Mchungaji Bo Ra Choi.

........................

Lakini anachosema Muhammad humo ni nini hasa?
 



Kifuatacho ndicho anachokisema Muhammad humo
kwa kilio kikubwa:
...........................
Mnajua mimi ni naniiiiiii?
Mimi ni Muhammad
Nilitenda dhambi kubwa sana
Nilifanya makosa makubwa mno
Nilikuwa mjinga
Nimetenda dhambi kubwa sana
Watu wengi sana wamekuwa wakitumbukia kuzimu kwa sababu yangu.
Nilitenda uhalifu mkubwa kuliko wote
Nilitenda dhambi kubwa kuliko zote
Nilitenda makosa
Nilitenda makosa
Yesu, nilifanya makosa.
Nilifanya hivyo kwa sababu nilikuwa maskini sana.
Nilitaka kuwa kiongozi wa watu wengi na nilitaka kuwa kama Yesu.
Nilifanya uhalifu mwingi sana wa kiovu
Niliua watu wengi sana
Msijikusanye pamoja
Mtakufa kama mkikusanyika kwa ajili yangu, Muhammad.
Tawanyikeni! Msijikusanye pamoja!
Kama mkijikusanya pamoja, shetani atawatumia!
Shetani atawatumia zaidi kama mkikusanyika kwa ajili ya Muhammad.
Bila ya Yesu, wote wanaishia kuzimu
Kuna joto kali!
Kuna joto kali!
Kuna joto kali!
Nitoe humu!
Nitoe humu!
Hakuna pepo ambayo mnaifikiria.
Kuna mbinguni na kuzimu tu.
Mafundisho hayo yamesambazwa kwa uongo. 
Uislamu umebadilishwa.
Haiwezekani!
Msipoteze maisha yenu namna hiyo.
Hakuna pepo ambayo Waislamu wanaiamini.
Mimi sikuzungumza juu ya mafundisho hayo ya uongo.
Yamebadilishwa.
Someni Biblia.
Inaonyesha namna ya kwenda mbinguni.
Hakuna mbingu katika Uislamu.
Mimi sikuandika theolojia hizo za uongo.
Mambo hayo yaliandikwa na watu waliokuwa wakijaribu kuniiga mimi.
Mambo hayo yamekuwa ni Biblia ya Uislamu ambayo inadhoofisha neno la Yesu.
Haiwezekani!
Sikuyaandika hayo!
Tafadhali, nisikilizeni!
Niko hapa kuzimu.
Niko hapa kwenye moto wa kuzimu.
Ninateseka kwa adhabu hii kubwa sana kwa sababu shetani alinitumia.
Msitupe maisha yenu kwa shetani!
Msiwe watii kwangu mimi, Muhammad.
Hiyo ni njia ya kwenda kuzimu.
Shetani atawatumia.
Tokeni humo kwenye Uislamu.
Mimi sikutaka haya.
Nilitaka tu kuwa mtawala wa taifa.
Lakini mambo yalienda vingine.
Hiki sicho nitakacho.
Sitaki vita.
Nilianzisha mapigano mengi ili kuunda taifa langu mwenyewe.
Mnajua ni kwa nini?
Ni kwa sababu nilikuwa maskini sana nilipokuwa mtoto.
Nilianzisha vita nyingi sana ili kuunda taifa langu.
Nilitaka tu kuongeza nguvu zangu ili kushinda vita.
Kwa nini Uislamu umebadilika hivyo?
Kama kweli mnataka kuwa watii kwangu,
Tawanyikeni na msiwasikilize viongozi wenu (wa dini).
Wanawaongoza kuelekea kwenye njia mbaya sana.
Wanaharibu maisha ya watu.

…………………………………….

Tafakari

Pima mambo

Chukua hatua